Ads

MSTAHIKI MEYA MANISPAA YA ILALA AKABIDHI MABATI 20 KATIKA OFISI YA CHAMA CHA MAPINDUZI KATA YA PUGU STATION.



Mstahiki Meya Manispaa ya Ilala amefanya ziara katika Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi ya kihistoria Pugu Station. Pugu Station ni miongoni mwa Kata ilitoka katika mikono ya Kata ya Pugu, Katika historia kulikuwa na kijiji cha Pugu ambapo hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alifungua Ofisi ya Ccm katika Kijiji cha Pugu.

Katika ziara yake hiyo Mstahiki Meya Mhe. Omary Kumbilamoto aliambatana na Katibu Siasa na Unezi Wilaya ya Ilala Cde. Said Side.

Mstahiki Meya Manispaa ya Ilala Mhe Omary Kumbilamoto amempongeza Mwenyekiti wa Vijana Kata ya Pugu Station Cde. Juma Mizungu kwa kutoa msukumo mkubwa kwako ili kukarabati Jengo hilo.
"Nampongeza sana Mwenyekiti wa Vijana wa Kata ya Pugu Station Cde. Juma Mizungu amefanya jitihada kubwa sana katika kuleta bati hizi amenieleza changamoto ya Kata hii na kunipa Msukumo nilete hizi bati" Omary Kumbilamoto

Baada ya kuona hali ya Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi Kata ya Pugu Station Katibu Siasa na Unezi Wilaya ya Ilala Cde. Said Side alimtaka Mstahiki Meya kuongeza mchango wake kwani uhitaji wa jengo hilo ni Mkubwa, Cde. Said Side ameitaka kamati ya Siasa pamoja na Diwani wa Kata ya Pugu Station wanaikarabati Ofisi.

Mstahiki Meya ameahidi kuikarabati Ofisi hiyo ya Chama Cha Mapinduzi Kata ya Pugu Station kwa kuweka tails pamoja na Gypsum,Tv pamoja na King'amuzi.

Leo la kufanya hivyo ni kuhakikisha Ofisi za Ccm zinakuwa katika hadhi kubwa.

No comments