HUDUMA ZA HYATT REGENCY HOTEL ZAREJEA.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo amezindua zoezi la utoaji wa huduma kwenye Hotel ya Kimataifa ya Hyatt Regency baada ya hotel hiyo kusitisha kutoa huduma kipindi cha nyuma kutokana na Janga la Corona.
RC Makonda ametoa wito kwa Wananchi na Watalii wote wanaoingia nchini kushukia katika hotel hiyo kwakuwa amejiridhisha na namna hotel hiyo imezingatia kanuni na taratibu zote zilizotolewa na Wizara ya afya ikiwemo wingi wa vitakasa mikono na barakoa.
Aidha RC Makonda amesema kitendo cha hotel hiyo kuendelea kutoa huduma pia itasaidia Serikali kupata kodi na ajira kwa wananchi huku akiwasisitiza wenye Hotel, Lodge, Bar, migahawa na maduka kuyafungua na kutoa huduma kama zamani.
Pamoja na hayo RC Makonda huu ni wakati wa kuendelea kuinua uchumi wa Nchi hivyo ametoa wito kwa wananchi kuchapa kazi kwa kiwango cha hali ya juu.
Post a Comment