Serikali yaeleza Mradi Bomba Mafuta Ghafi EACOP
SERIKALI ya nchini imetoa taarifa kuu iliyo wasilishwa na kujadiliwa pamoja katika eneo la Ziwa Albert nchini Uganda pamoja na maendeleo ya mradi wa bomba hilo la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP)
Hivyo katika malengo hayo imeiomba kampuni ya ujenzi wa mradi huo iitwayo Total East Africa Midstream B.V(TEAM BV) kukamilisha ujenzi wa mradi huo kabla ya miezi 36 ya mkataba.
Hayo yamesemwa Dar es Salaam na Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani katika kikao chake na kampuni hiyo kilichoitaarifu serikali maendeleo ya mradi katika eneo la Ziwa Albert nchini Uganda pamoja na maendeleo ya mradi wa bomba hilo.
"Tayari kampuni ya Total imekamilisha makubaliano mapya ya kampuni ya Tullow kununua hisa zake katika mradi wa eneo la Ziwa Albert ," alisema Dtk.Kalamani.
Alisema shughuli za ujenzi zitaanza mapema mwakani , nimewaomba wakamilishe hatua chini ya miezi 36 ya mkataba .
Alisisi tiza kuwa litakuwa na uwezo kutoa mapipa 236,000 ambapo litaimarisha Bandari ya Tanga kimapato baada ya muda kumalizika
Amemshukuru Rais Dkt.John Magufuli pamoja na Rais wa Uganda ,Yoweri Mseveni kwa kufanya majadiliano yaliyo fanikisha kuendeleza mchakato wa ujenzi wa bomba hill.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uchimbaji na uzalishaji wa TEAM BV , Arnaud Breuillac alisema wameitaarifu ,wizara hiyo hali ya mabadiliko makubwa kiuchumi dunia itailazimu kufanya maboresho katika ofa za zabuni mbali mbali ili kulingana na matakwa mapya ya soko.
Post a Comment