KATE KAMBA ,AFUNGUKA MCHANGO WA KUMBILAMOTO , UJENZI OFISI YA CCM KATA YA VINGUNGUTI.
Mwamba wa habari
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es salaam , Mama Kate Kamba amewataka viongozi wa chama na Serikali kuacha alama katika uongozi wao bila kujali vyeo walivyo navyo .
Kamba aliyasema hayo Wilaya ya Ilala alipofungua Jengo la Ofisi za Chama Cha Mapinduzi Kata ya Vingunguti lililo karabatiwa na Diwani wa kata hiyo ambaye pia ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Mhe Omary Kumbilamoto.
'' Niwapongeze sana kata ya Vingunguti na Wilaya ya Ilala kwa kutumia akiba yenu ya milion 12, kufanya ukarabati lakini pia kumshukuru Mstahiki Meya kwa kutumia uzoefu wake wa kusaidia pale anapo toka amejitoa na kusaidia pale anapotoka hii inatufundisha na sisi wengine pale tulipo tuta acha alama gani? tujitahidi sana kuacha alama na lama hiyo inaweza ikawa jengo au vikundi kuviimarisha kusaidia kuongeza uchumi"Alisema Kamaba
Pia Mwenyekiti huyo alitembelea Mradi wa kimkakati wa Machinjio ya Kisasa inayojengwa na Serikali ya awamu ya katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na amewapongeza wasimamizi wa Mradi huo na Shirika la Ujenzi Shirika la nyumba ta Taifa (NHC) kwa kujenga kwa viwango na gharama nafuu.
Aidha aliwataka wakazi wa Vingunguti na Watanzania kwa ujumla kutumia fursa hiyo kuanzisha viwanda vidogo vya kupaki nyama kwenye makopo ili kuongeza ajira .
"Tunauziwa nyama za makopo kutoka uarabuni na nchi zingine ilihali Tanzania ndiyo tuna mifungo mingi kuliko hizo nchi tujitahidi sana kuwekeza na sisi tuuze nyama nje "Alisema
Hata hiyo kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika oktoba mwaka huu amewatahadhalisha wana CCM na wanacham kujiepusha na kutoa na kupokea rushwa kwani wakibainika watachukuliwa hatua za kisheria .
Pamoja na hayo Mwenyekiti huyo aliwapokea Wanachama wapya waliotoka Chama cha Wananchi (CUF ) walioamua kujiunga na Chama cha Mapinduzi zoezi lililoambatana na kukabidhi Jezi kwa vijana wa Hamasa wa Kata ya Vingunguti zilizo tolewa na Diwani wa kata hiyo Omary Kumbilamoto.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto ambaye kwa kiasi kikubwa amechangia ukarabati huo,alisema anamshukuru Mungu kwa kufanikisha ukarabati huo na kuwashukuru wadau wote walio muunga mkono .
"Nilipo ingia udiwani nilijiminya hela yangu nikanunua TV nikawapa Zahanati ya Vingunguti maana walikuwa wanahangaika sana ,pia nikanunua Jenereta sasa hakuna shida ya umeme,nilinunua pia Gari la wagonjwa,pia niliweka patition za wodi za wagonjwa ,ndugu mwenyekiti mimi kwa muda wa miaka yote mitano nilikuwa nasaidia tu sasa namimi ndo nimeanza kujenga ofisi yangu"Alisema Kumbilamoto.
Post a Comment