TAKUKURU MKOA WA ILALA YATOA ONYO KWA WAGOMBEA
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akimkabidhi cheti cha Shukrani Diwani wa Kata ya Kata ya Ilala Saady Kimji,vyeti hivyo vimetolewa na Mkurugenzi wa manispaa ya Ilala
Afisa Mchunguzi Mwandamizi wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Ilala Elly Makala akizungumza katika Baraza la madiwani
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ilala Jumanne Shauri akifungua kikao cha Baraza la madiwani Leo Juni 10/2020 (kushoto) Meya wa Ilala Omary Kumbilamoto
NA HERI SHAABAN
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Ilala imetoa onyo katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais Wabunge na Madiwani amewataka wanasiasa wa vyama mbalimbali wasitumie rushwa katika kusaka uongozi .
Hayo yalisemwa katika Baraza la Madiwani halmashauri ya Ilala leo, na Mchunguzi Mwandamizi wa TAKUKURU Elly Makala wakati wa kuwasilisha taarifa kwa madiwani mtu anapofanya kampeni kwa rushwa na madhara yake.
"TAKUKURU jukumu letu kutoa elimu kwa wananchi hatukamati mtu tukipata taarifa kwanza tunafanya uchunguzi tukijilidhisha ndio tunamkamata hivyo ukifanya kampeni inatakiwa ufanye kwa uwazi na kujiamini bila kutoa rushwa "alisema Makala.
Aliwataka wagombea wote kujiamini ili aweze kupatikana kiongozi bora kwa ajili ya maendeleo na kuisaidia Serikali.
Aidha Afisa TAKUKURU alitoa onyo kwa wagombea kujitoa dakika za mwisho kwa ajili ya kuchukua rushwa ili asigombee nafasi yake aliyoomba ridhaa kwa wananchi.
Alisema ukitenda kosa uwezi kugombea aliwataka wasitumie Mamlaka yao vibaya au kugharamia wanachama wa vyama vyao katika maswala ya chakula au usafiri bila bila ridhaa ya Chama.
Pia aliwataka wasitoe fedha kwa ajili ya kupata nafasi ya uteuzi,uchaguzi ni demokrasia maadili ndio jambo la msingi katika kuelekea uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na madiwani .
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilala Dkt. Sophia Mjema amewapongeza madiwani wake wa Ilala, Wakuu wa Idara, Watendaji na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kwa utendaji mzuri wa kazi na ushirikiano walio onyesha katika kipindi cha uongozi wa Rais John Magufuli ambapo Ilala imefanya vizuri kusimamia mapato, elimu na utoaji wa mikopo.
Dkt Sophia Mjema aliwapongeza pia kwa ushirikiano waliotoa watendaji wa Ilala na madiwani wakati wa ziara za kutatua kero za wananchi kata kwa kata Majimbo yote ya Wilaya ya Ilala.
Akizungumzia Barabara mbovu Dkt, Sophia Mjema alisema fedha zipo za kutosha barabara zote Wilaya ya Ilala zitajengwa tuendelee kumuunga mkono Rais John Magufuli katika kujenga Tanzania ya uchumi wa katika kusimamia miradi yote ya Maendeleo.
Naye Meya wa Halmashauri ya Ilala Omary Kumbilamoto alisema fedha zilizotengwa kwa ajili ya Barabara ya Kimanga Jimbo la SEGEREA zitumike kama ziivyopangwa zisipelekwe katika miradi mingine wananchi wa Kimanga wamepata kero ya barabara muda mrefu.
Pia Meya Kumbilamoto alisema hospitali ya Wilaya ya Ilala imeanza kazi na leo wamama wanne wamejifungua katika hospitali hiyo amewataka wananchi kuitumia kwa ajili ya huduma.
Post a Comment