Ads

BENKI YA TPB YAPATA FAIDA YA SHILINGI BILIONI 15.9


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya TPB Dkt. Edmund Mndolwa,(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani Jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, wakati wakutoa tarifa ya kupata faida ya kodi ya Shilingi Bilioni 15.9 kwa mwaka Desemba 2019. Ambaye Mkutano Mkuu wa 28 wa wanahisa wa Benki hiyo ya TPB. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Sabasaba Mushingi.



Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB Sabasaba Moshingi,(kulia) akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani Jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki wakati wa kutoa tarifa ya kupata faida ya  kodi ya Shilingi Bilioni 15.9, kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Benki ya TPB, Dkt. Edmond Mndolwa.


Baadhi ya viongozi mbalimbali wa benki hio wakibadilishana mawazo katika mkutano mkuu wa 28 wa wanahisa wa Benki hiyo ya TPB wakati wa kutolewa tarifa ya kupata faida ya kodi ya shilingi Bilioni 15.9 kwa mwaka Desemba 2019.

Mwamba wa habari

BENKI ya TPB imepata faida ya baada ya kodi ya Shilingi bilioni 15.9 kwa mwaka unaoishia 31 Desemba 2019.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Dkt. Edmund B. Mndolwa, aliwaambia waandishi wa habari wakati wa Mkutano Mkuu wa 28 wa Wanahisa wa Benki hiyo kuwa Benki ya TPB imeendelea kuimarika kwa kutengeneza faida kubwa hadi kufikia faida kabla ya kodi ya Shilingi bilioni 23.0.

“Mafanikio haya yaliyopatikana kwa mwaka 2019 yanatokana na juhudi kubwa iliyofanywa na Menejimenti na wafanyakazi chini ya ushauri wa karibu wa Bodi ya Wakurugenzi katika utendaji kazi wa kila siku na kujituma kwa wafanyakazi wote kwa ujumla”.

Dkt. Mndolwa akasisitiza kuwa ingawa Benki ya TPB ina mtaji mdogo ukilinganisha na benki zingine, lakini wameweza kufanya vizuri kwa takribani miaka minne mfululizo kwenye sekta ya benki nchini.

Kutokana na faida nzuri iliyopatikana kwa mwaka 2019, Benki inatarajia kutoa gawio la fedha taslim kwa wanahisa wake ikiwa ni sehemu ya faida iliyopatikana.

Hii ni kulingana na sera na taratibu ambazo Benki imejiwekea ili kuendelea kuimarisha uendeshaji wake lakini pia kugawa sehemu ya faida kwa wanahisa.

 “Nina imani wanahisa wote watafurahia kupata gawio la fedha taslim ambapo kwa mwaka huu litaongezeka ukilinganisha mwaka uliotangulia kwa kadri Benki inavyoendelea kujiimarisha na kutengeneza faida kubwa zaidi”, aliongeza Dkt. Mndolwa.

Faida iliyopatikana mwaka 2019 inatajwa na uongozi wa benki kuwa ni kubwa ambayo haijawahi kufikiwa tangu kuanzishwa kwa Benki ya TPB takriban miaka 95 iliyopita.

Alisema kwamba benki hiyo itaendelea kujipanga na kupanua shughuli zake za kibenki nchini na kuweka mikakati madhubuti ya kukabiliana na changamoto za kiuchuni kwa sasa katika sekta ya fedha nchini.

“Napenda kuchukua fursa hii kuwasihi wateja wote na watanzania wote kwa ujumla pamoja na taasisi mbalimbali kuendelea kuitumia Benki ya TPB katika kuiunga mkono kwenye shughuli zake ili iweze kutimiza malengo yake vyema”, alihitimisha Dkt. Mndolwa.

No comments