WANANCHI WAMETAKIWA KUENDELEA KUCHUKUA TAHADAHARI YA CORONA ISIENDELEE NCHINI.
Mwambawahabari
Ikiwa ugonjwa wa Covid_19 kuendelea kupungua nchini, Shirika la Elimu ya Utunzaji wa Amani (EA) limewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ili ugonjwa huo usiendelee kuenea.
Wito huo umetolewa leo Jijin Dar es salaam na Mwenyekiti wa Kanda ya Mashariki na Pwani wa Shirika la Elimu ya Amani Abdul Ibrahimu wakati akimkabidhi msaada wa Vitakasa Mikono (Sinitizer) Mkuu wa Kituo cha Polisi Chang'ombe Kamanda Dastan Kombe.
Amesema watu wanatakiwa kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Covid_19 ili kusaidia ugonjwa usiendelee kuenea na kuleta athari zaidi.
"Leo tumetoa msaada wa vitakasa Mikono kwa Kituo cha Polisi Chang'ombe ikiwa na lengo ni kuunga mkono Juhudi za Serikali katika kupambana na virusi vya Korona tunatambua kuwa ugonjwa wa Korona umepungua lakini ni jukumu letu kuhakikisha tunajihadhari na ugonjwa huu ili uendelee kupungua na kupotea." Alisema.
Yusuph Jumanne ni Mwenyekiti wa Wilaya ya Temeke wa Shirika la Elimu ya Amani amesema wataendelea kutoa hamasa na watu kufuata taratibu za afya kwa kuwasisitiza watu kuvaa barakoa na kunawa Mikono Kama ambavyo Serikali na wataalamu afya walivyoelekeza ili ikiwa katika jitihada za kuzuia na kupambana na ugonjwa huo.
"Sisi kama Shirika la Elimu ya Amani hatutaacha kusisitiza uvaaji barakoa na kunawa mikono Kama ambavyo tumeweza kuanza kutoa elimu maeneo ya Mbagala kuhamasisha watu kuvaa barakoa kwenye daladala na watu wametoa ushirikiano kwa kukubali kuvaa barakoa ikiwa ni njia mojawapo ya kujikinga na Virusi vya Korona." Amesema.
Kwa upande wake Mkuu wa Kituo Cha Polisi Chang'ombe Dastan Kimbe ameishukuru Shirika la Elimu ya Amani kutoa msaada wa vitakasa Mikono kwa Kituo Cha Polisi Chang'ombe ikiwa katika madhumuni ya kuwasaidia kupata Sabuni ya kunawa mikono ambayo itawasaidia kuitumia katika mchakato kwa mapambano ya ugonjwa wa Korona.
"Tunashukuru Shirika la Elimu ya Amani kutoa msaada wa vitakasa Mikono ikiwa ni katika juhudi za kuisaidia Serikali kupambana na kudhibiti Virus vya Korona." Amesema.
Post a Comment