Ads

TCRA yawanoa Kamati ya Amani Mkoa wa Arusha


Na Mwandishi Wetu Arusha
Mkuu wa Mkoa  wa Arusha Mrisho Gambo amesema Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)  imechagua kundi sahihi la viongozi wa dini kwa ajili ya kuwapa elimu ya mawasiliano.

Gambo ameyasema hayo wakati wa semina ya Kamati ya Amani Mkoa Arusha, amesema viongozi wa dini wana nafasi kubwa ya kutoa elimu kwa waumi juu ya kujikinga na uhalifu unapotumia huduma za mawasiliano.
Amesema kuwa watu watumie mawasiliano kwa kuzingatia uzalendo pamoja na kutumia mawasiliano katika kujenga uchumi wa nchi.

"Naamini viongozi wa  dini mtafikisha elimu hii kwa ufasaha na kujenga taifa lenye maadili mema katika utumiaji wa mawasiliano"

Amesema kampeni ya Sirubuniki Mjanja Haingizwi Chaka ni kampeni ambayo imeanza kwa kundi  la Viongozi wa dini ikiwa ni kundi lenye watu wengi na rahisi kutoa elimu ya kujikinga na uhalifu unapotumia huduma za mawasiliano.
Aidha amesema kuwa katika ukuaji wa sekta ya mawasiliano ni vyema kuwa wabunifu wa kutumia mawasiliano kwa kuhabarishana habari za kujenga maadili.

Mkuu wa Kanda ya Kaskazini Mhandisi Emelda Salum, amesema viongozi wa dini kuwa ngazi  katika kufikisha elimu kwa haraka kutokana na kuwa na kundi kubwa la waumini wa rika zote.

Mhandisi Salum amesema  kuwa semina ya viongozi wa dini italeta mafanikio kwa wananchi kuwa na uelewa namna ya kutumia mawasiliano.

Aidha  amesema kuwa Kanda ya Kaskazini  itaendelea kutoa Elimu ya Mawasiliano katika Kujikinga na uhalifu unapotumia huduma za mawasiliano.

Kampeni  ya Sirububiki Mjanja haingizwi chaka  inalenga kuzifikia kamati za Amani za mikoa yote ya Tanzania

Kamati za Amani za mikoa ni kamati za viongozi wa dini na madhehebu  mbalimbali ambazo zimeundwa kwa lengo  la kujenga  maridhiano kwa watu wa dini mbalimbali.

Nae Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TCRA Mabel Masasi, amesema kuwa wanafikia makundi yote katika Kampeni ya Sirubuniki  Mjanja Haingizwi Chaka.

Amesema wakati  umefika  wa kutumia mawasiliano kwa kulinda usalama wa nchi.

No comments