Ads

WAJUMBE WAMPA ASILIMIA 100 ADO SHAIBU KATIBU MKUU ACT- WAZALENDO

Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama ACT Wazalendo wamemchagua ndugu Ado Shaidu kuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho baada ya kupata asilimia 100 ya kura zote katika uchaguzi uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Wajumbe wa mkutano huo wameonekana kuwa na furaha baada ya matokeo kutangazwa, Ado Shaibu kabla ya kuchaguliwa kuwa katibu alikuwa katibu Mwenezi wa chama hicho.

Viongozi wengine waliochaguliwa ni pamoja na Bw. Zitto Kabwe amechaguliwa kuwa kiongozi Mkuu wa Chama, Bw. Juma Haji ni makamu mwenyekiti upande wa Zanzibar, Bi Dorotha Semu ni Makamu mwenyekiti Tanzania bara.

No comments