RAIS MAGUFULI AKUTANA NA WANANCHI WA CHATO KATIKA KIJIWE CHA KAHAWA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ambaye leo tarehe 28 Machi, 2020 amewasili nyumbani kwake Chato Mkoani Geita akitokea Mkoani Dodoma amekutana na wananchi wenzake wa Chato katika kijiwe cha Kahawa na soko la maboga na kuwapongeza kwa juhudi za kujitafutia kipato.
Mhe. Rais Magufuli ameonekana akifurahia kukutana na wananchi wenzake huku wakinywa kahawa pamoja na amewatembelea akina Mama wanaouza maboga na kununua maboga hayo kwa ajili ya chakula chake cha nyumbani.

Post a Comment