APANDISHWA KIZIMBANI KWA KOSA LA KUOMBA RUSHWA
Mwambawahabari
Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Kinondoni(TAKUKURU) Leo inatarajia kumfikisha mahakamani Amos Joseph Uisso(30) mkazi wa Bunju na mtumishi wa Kinondoni football Association (KIFA) katika mahakama ya Kinondoni kwa kosa la kuomba rushwa ya sh.500,000 na kupokea sh.330,000 ambapo nikinyume na kifungu cha 15 (1) cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba11/2007.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Kinondoni Theresia Mnjagira amesema Novemba 18,2019 mtuhumiwa aliomba rushwa ili aweze kuipitisha timu ya Ndwumbwi kucheza ligi daraja la tatu kinyume cha utaratibu na sheria.
"Napenda kuwaasa vyama vya michezo, Vilabu,wachezaji,viongozi,makocha,marefa na mashabiki kuzingatia vigezo,taratibu na sheria katika kuendesha vyama vya michezo nchini ili tuweze kupata timu bora, Nawaasa wajiepushe na vitendo vya rushwa "amesema
Post a Comment