Ads

TAKUKURU MKOA WA KINONDONI YADHIBITI MIANYA YA RUSHWA ZAIDI YA SH.BILIONI 12 KATIKA KIPINDI CHA MWEZI OKTOBA HADI DISEMBA

asisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kinondoni imeweza kudhibiti mianya ya Rushwa katika miradi ya maendeleo tisa yenye thamani ya bilioni 12,217,537,000/= katika kipindi cha mwezi Oktoba hadi Disemba 2019, na kubaini kuwa kati ya miradi iliyokaguliwa mradi mmoja wenye thamani ya sh. milion(86,600,000/=) una viashiria vya Rushwa. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Kinondoni, Bi.Theresia Mnjagira amesema katika kipindi hicho kubwa lilielekezwa katika kudhibiti vitendo vya Rushwa kwenye Uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika tarehe Oktoba 24 mwaka jana kwa kuhakikisha wananchi wanapata elimu kuhusu madhara ya rushwa katika uchaguzi na umuhimu wa kuchagua viongozi waadilifu kwa maendeleo ya taifa. Aidha Bi.Theresia amesema kuwa TAKUKURU katika Mkoa huo imechukua hatua ya kuanzisha uchunguzi kwa mradi mmoja uliobainika kuwepo ukiukaji wa taratibu kwa lengo la kujua sababu za ukiukwaji huo pale itakapothibitika kuwa vitendo vya rushwa vimetendeka hatua stahiki zitachukuliwa. Hata hivyo Bi. Theresia amesema Takukuru Kinondoni itaendelea na majukumu yake ya kuelimisha umma,wanafunzi na wanavyuo ili kuimarisha madili kama njia ya kudhibiti rushwa. Pamoja na hayo ametoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Taasisi hiyo katika mapambano dhidi ya rushwa.

No comments