SERIKALI IMEWEKA MAZIGIRA WEZESHI KWA WAFANYABIASHA NA WANAOWEKEZA VIWANDA NCHINI.
Serikali imesema imeweka mkakati maalumu ili kuimarisha na kuendeleza Sekta ya Viwanda , kuongeza ajira , kupunguza umaskini kwananchi wake .
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Mhandisi Stella Manyanya wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Nne ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yaliyoanza tarehe 5 hadi 9 Desemba, 2019 katika Uwanja wa Maonesho wa Mwl J.K.Nyerere na kufafanua kuwa Serikali itaendelea kuwalinda wawekezaji wote wanaoamua kuanzisha viwanda hapa nchini kwa kuwapatia vivutio maalumu ikiwa ni pamoja na kuweka mazingira muafaka ya uwekezaji na biashara.
"Tuta kuhakikisha kuwa bidhaa zisizo na viwango na bandia hazitakuwa na nafasi katika soko la Tanzania, hivyo ni muhimu kuhakikisha bidhaa zinazoingia nchini zinakuwa na viwango vya kimataifa ili kuvipa changamoto viwanda vya ndani kuzalisha bidhaa zenye ubora" Alisema
Aidha amewaomba wawekezaji kuendelea kuwekeza Tanzania kwasababu ina maeneo mazuri ya kujenga viwanda, fursa za malighafi na kuna walaji wa kutosha .
Aliongeza kuwa, serikali ya Tanzania inatambua na kufahamu umuhimu wa mazingira wezeshi kwa mfanyabiashara na mwekezaji wa viwanda, imechukua jukumu la kuweka miundo mbinu wezeshi kwa kuhakikisha kwamba umeme unapatikana ndio maana inajenga mradi mkubwa wa uzalishaji wa umeme katika maporomoko ya mto Rufiji takriban megawat 2500 vilevile kuna umeme ulioongezwa pale Kinyerezi na kuchangia ongezeko la takriban megawatt 1600 na kufanya nchi yetu kuwa na umeme wa kutosha hivyo kiwanda kinaweza kuanzishwa sehemu yoyote
Pia serikali imeendelea kuondoa mikanganyiko ya kodi na mikanganyiko ya taasisi za udhibiti kwa kuhakikisha kuwa inapunguza kodi na mpaka sasa kodi takribani 168 zimeondolewa kwaajili ya kuweka mazingira wezeshi na Mamlaka nyingi kama vile Taasisi ya Tume ya Ushindani (FCC) na nyingine zote zinazohusika na ukaguzi zinazingatia bidhaa zinazoingia nchini zinakuwa bidhaa halisi na haziui soko la ndani.
Aliongeza kwa kusema kuwa kama ambavyo ilivyo kwenye dira ya Taifa, ifikapo 2025 tunatamani kuona Tanzania inafikia uchumi wa kati lakini kufikia hapo ni pale taasisi za serikali zitakapokuwa na msimamo mmoja kuhakikisha kwamba tunaisaidia sekta binafsi ambao ndio watekelezaji na watendaji katika uzalishaji na kuwezesha upatikanaji wa uzalishaji wenye tija na kufanya bidhaa zetu ziwe na bei zinazoweza kumfikia mlaji na hivyo kukuza uchumi wetu.
Ametoa rai kwa wadau na washiriki wanaoonesha bidhaa zao kuhakikisha kila wanachozalisha wanazingatia ubora unaostahili na amelitaka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Viwanda (UNIDO) kufadhili mradi wa kuunda kanzidata ya viwanda vinavyoanzishwa na vinavyokuwa kwa gharama nafuu.
Kwa upande wake Dkt Stephen Kargbo, mwakilishi wa UNIDO nchini alisema kuwa uwepo wa siku ya viwanda vya ndani ni muhimu kwani hufanya kujua changamoto ambazo watu wenye viwanda wanakutana nazo na ni fursa kwa wadau kubadilishana mawazo kuhusu viwanda na njia bora za kutumia jambo ambalo linaloakisi ukuaji na ushirikiano katika nchi za Afrika na kuongeza kuwa katika kuendeleza muingiliano wa kibiashara katika nchi ya Afrika soko la pamoja la AFCFTA linatarajiwa kuongeza ushindani na kusisimua sekta ya uzalishaji
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya (TanTrade) Dkt Ng’wanza Kamata, aliwashukuru washiriki wa Maonesho hayo kwa kuitikia wito wa kuja kushiriki na amesema kuwa uongozi wa Serikali ya awamu ya Tano Serikali ya Awamu ya Tano inasisitiza na imekuwa ikitilia mkazo viwanda.
Post a Comment