Ads

Mwanamke wa kwanza nchini kumiliki kiwanda cha rangi atoa neno kwa watanzania

Naibu waziri wa viwanda na Biashara Mhandisi Stelah Manyanya akiwa na mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Platnum Paints Investiment Company (LTD) Bi Mange Shayo, alipo tembelea banda hilo katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Sabasaba)
Na John Luhende
Mwamba wa habari
Watanzania wametakiwa kujenga utamaduni wa kupenda kutumia bidhaa zinazo zalishwa na viwanda vya ndani ili kujenga uchumi wanchi na kuongeza ajira kwa vijana.

Hayo yamebainishwa na mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Platnum Paints Investiment Company (LTD) Bi Mange Shayo , katika maonesho ya bidhaa za viwanda vya ndani yanayo endelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Sabasaba) ambapo amesema kunabaadhi ya watanzania wamekuwa na imani zaidi na bidhaa zinazozalishwa nje ya nchi jambo ambalo amesema halinatija kwa Taifa.

"Nataka niwaambie watanzania wenzangu bidhaa zinazo zalishwa hapa nchini nibora sana tena kuliko hata zile zinazo zalishwa nje ,nashukuru kunabaadhi wameanza kuelewa na mimi nashukuru tuna biadhaa yetu ya Rangi za kupaka majengo inaitwa Platnum , wameisifia sana naomba nawengine watuunge mkono"Alisema Mange

Aidha ameishuku Serikali kwakuwasaidia wajaisilamali wandani hasa kwa kuandaa maonesho ya biashara yanayo wasidia kujitangaza ikiwemo kuweka mazingira wezeshi kibiasha .
''Namshukuru sana Naibu waziri wa viwanda na Biashara Mhandisi Stelah Manyanya kwa kututembelea katika maonesho haya pia napenda kutumia fursa hii kumshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kaulimbiu yake ya viwanda kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda imetuhamasisha sana"Alisema

Mkurugenzi huyo pia amewatia moyo wajasiliamali wanawake ambapo amesema yeye ni mwekezaji wakwanza mwanamke nchini kuanzisha kiwanda cha rangi na kuweka wazi kuwa alianzia mbali kama mpambaji kisha kuwa na kampuni ya Printing na sasa ameanzisha kiwanda cha rangi .

"Nilipo aliamua kuanzisha hii kampuni nilikaa nikafikiria nikaona katika Tanzania hakuna mwekezaji mwanamke mwenye kiwanda cha rangi nikajaribu kuangalia nikaona viwanda vya rangi vyote ni vya watu kutoka nje au wahindi , nikaamua kuwaunga mkono watanzania na wanawake wenzangu waone kuwa wanawake tunaweza"Alisema

1 comment: