Ads

LAMI YA MAJI KUTATUA CHANGAMOTO ZA MIUNDO MBINU KWA GHARAMA NAFUU.



Na John Luhende
Mwamba wa habari
Gharama za ujenzi wa barabara za lami hapa nchini zinztarajiwa kushuka chini baada ya kukamilika kwa utafiti na majaribio ya lami ya maji isiyo tumia mafuta.

Hayo yamebainishwa na afisa masoko wa kampuni ya STAPECO , John Simkoka , alipokuwa katika maonesho ya 4 ya bidhaa za viwanda vya Tanzania ambapo amesema kwa sasa wako katika majribio baada ya kuwasilisha formular kwa wataalamu wa chuo kikuu cha Dar es salaam.

"tumefanya majaribio haya katika bara bara za changanyikeni ,Kileleni na ukombozi , tumekarabati na nyingine tumetengeneza lami upya kama mita 120 mpaka sasa inamuda wa miezi mitatu tukisha maliza majaribio haya tutakabidhi matokeo ofisini serikalini ili ikabidhiwe TANROAD na TARURA na kuwapa wakandarasi waanze kuitumia "Amesema.

Alisema Lami hii inafaida kubwa kwanza mi rafiki wa mazingira kwa kuwa haitumii mafuta maji ni rahisi kuyapata na sigharama kama mafuta , pia haihitaji kukata misitu ili kuchemsha kama ilivyo lami ya mafuta .

Faida nyingine aliyo itaja ni kusaidia kukua kwa makampuni ya wakandarasi wazawa ambao hawana mitaji mikubwa wala kiwanda cha kuchemsha lami hivyo ita saidia kuongeza miundo mbinu bora ya barabara kwa gahara nafuu na itaongeza ajaira kwa vijana na watanzania kwa ujumla.

Hata hivyo ameishukuru Serikali kupitia Tume ya Sayansi na Teknolojia kwa kuwapatia fedha kwaajili ya kutekeleza wazohilo kulitoa katika makaratasi na kulifanya kwa vitendo.
Kwa upande wake kaimu afisa habari wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Deusidedith Leonard amesema ,Tume hiyo imekuwa ikiwasaidia wabunifu kuhifadhi na kuendeleza bunifu zao.

"Mtaalamu huyu kaja na tekonolojia yake nzuri na sisi tumeipokea tunamsaidia kuiendeleza tunarajia kwamba pindi majaribio haya yaki kamilia yataisaidia nchi kuokoa fedha nyingi kutoka kwa makampuni makubwa ya ncje ambayo yanajenga bara bara za lami kwa kwa gharama kubwa"Amesema.


No comments