Diwani Mtarawanje atoa ushauri mzito kwa wahitimu wa vyuo vikuu.
Na John Luhende
Wahitimu wa vyuo vikuu hapa nchini wametakiwa kuitumia elimu yao kwa kubuni na kuzalisha vitu vipya badala ya kutegemea kuajiriwa pekee huku wakiacha kuifanyia kazi elimu ya kujitemea.
Hayao yamebainishwa na Diwani wa kata ya Kijichi Eliasa Mtarawanje wakati akizungumza na waandishi wa habari katika mahafali ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania ( TIA) ambapo naye alikuwa mmoja wa wahitimu wa shahada ya Manunuzi na Ugavi, ambapo alisema Elimimu waliyoipata inatosha kwenda kuzalisha ajira badala ya kusubiri kuajiriwa.
"Msisitizo huu wakati ukitolewa mimi nilikuwa niko chuoni na hili mimi nimelifanyia kazi ndiyo maana unaona nasoma lakini huku nikitumikia katika nafasi ya diwani , na baadhi ya wenzangu ambao wamehitimu wana shughuli zao "Alisema.
Adha amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kuwapa nafasi vijana katika utumishi kwa kuwateuwa katika nafasi mbali mbali katika chama na Serikali na kusema kuwa yeye na vijana ambao wamepewa dhama ya kumwakilisha katika nafasi watafanya kazi kama timu ili kufanikisaha malengo na maendeleo kwa wananchi.
"Namshuku sana Rais Magufuli kwa ktuamini vijana ameteuwa vijana katika nafasi z
a ukurugenzi ,mkuu wa Wilaya na mikoa tofauti na hapo mwanzo hatukupewa sana nafasi na mmeona vijana wamesoma na wanafnya kazinnzuri ila taswira ilionekana kama vijana hawawezi kuaminika yeye kafuta wazo hilo naomba vija wenzangu wanaofanya kazi na watakoa pewa dhama ya kutumika wananchi wawe waaminifu na waoneshe imani "Alisema
Pamoja na hayo Mtarawanje amewashauri vijana wasomi kujitokeza katika nafasi za kugombea na kuwataka wale amboa hawana elimu kubwa kujiendelea ili kuenda na wakati.
'Nikweli Diwani anaweza kugombea kwa kuwa na sifa ya kujua kusoma na kuandika lakini nataka niwa shauri kujiendeleza ni muhimu ili kukabili changamoto zilizopo wenzetu wako mbali sana mfano mimi nilienda kwenye mkutano wa ICPD kule Nairobi washiki kutoka sehemu nyingine walioneka wako vizuri zaidi kuliko waliotoka Africa Mashariki katika uelewa wa mambo na kuzungumza lugha ya Kiingereza"Alisema
Post a Comment