Ads

Meya Ilala awashukuru wadau mbele ya wananchi Vingunguti , baada ya mchango wao katika shughuli za maendeleo.

Na John Luhende
Mstahiki Meya  wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto amewashukuru  wadau wamaendeleo waliojitolea kulisha chakula  shule za msingi katika kata ya Vingunguti na kusema msaada huo imesaidia kuongeza kiwango cha elimu.


Meya Kumbila ameyasema hayo akiwa katika mkutano wa hadhara  uliofanyika vingunguti  ukiwa na lengo la kuwaeleza wananchi mafanikio ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika sekta  mbalimbali ikiwemo afya ,elimu  na miundo mbinu ambapo akizungumzia elimu amesema ufaulu wa wananfunzi  umeongezeka  ambapo  wanafunzi  1035 wamefaulu na zaidi ya 23000 katika Manispaa.
Kufuatia mchango huo  amewapa vyeti maalumu vya kuwatambua katika ushiriki wao katika kuungamkono elimu  bure inayoyo tolewa na serikali ya awamu ya tano , wadu hao ni TPTL,wanatoa  madawati 50 katika shule ya msingi mtakuja , Education for big result, wamejenga vyumba   vya madarasa na vyoo shule ya msingi kombo , pia wametoa majokofu katika shule mbili na zahanati ya Vingunguti.
Aidha akizungumzia mafanikio katika sekta ya afya  amemshukuru Rais Magufuli kwa kukiwezesha kituocha afaya Mnyamani kwa kukiboresha na  kuongeza vifaa tiba ambapo  jumla ya shilingi milion 177 ametoa katika kituohicho.
Kumbilamoto akieleza maendeleo ya ujenzi wa machinjio ya kisasa Vingunguti, na kusema kuwa  wafanyabiashara na Mamalishe waliokuwapo tangumwanzo watapewa kipaumbele baada ya ujenzi kukamilika.
''Sitaki kuwe na upendeleo wa kuwekana ndugu au wajomba  katika machinjio hii ,tutawatengenezea eneo lao maalumu na wachinjaji waliopo watapewa mafunzo ya kutumia mashine maalumu za kuchija mifugo.



Pamoja  ametoa  jezi kwa vikundi viwili  vya Jogging , na Tv moja katika ofisi ya CCM  kata ya vingunguti  ,ambapo katibu wa CCM kata ya Vingunguti Agath Limbumba amemshukuru diwani huyo kwa msaada huo.


No comments