CUF YATANGAZA KUTOSHIRIKI UCHAGUZI SERIKALI ZA MTAA.
Chama Cha Wananchi (CUF) kimejiondoa kushiriki uchaguzi wa serikali za mtaa unaotarajia kufanyika Novemba 24 mwaka huu.
Akitangaza maamuzi hayo leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba, amesema hawawezi kushiriki uchaguzi wakati asilimia kubwa ya wagombea wao wameongolewa.
"Hatuwezi kushiriki uchaguzi, na wagombea wachache waliobaki wanatakiwa kuandika barua ya kutoshiriki uchaguzi, kazi iliyobaki ni kukijenga chama, watakaotangazwa sio viongozi halali" amesema Prof Lipumba.
Post a Comment