Ads

Benki Ya Mkombozi Yatangaza faida Ya Bilioni 1

Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Mkombozi Profesa Marcellina Mvula Chijoriga akizungumza na waandishi wya habari leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Mkombozi, Bw. Thomas Enock.
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Benki ya Mkombozi imejipanga kufanya maboresho makubwa katika utendaji ikiwemo kuweka miundombinu ya kidigitali pamoja kuendelea kutoa mikopo kwa wajasiriamali.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaaam wakati akitoa ripoti ya robo tatu, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Mkombozi, Bw. Thomas Enock, amesema kwa katika miezi mitatu ya mwanzo wamefanikiwa kufungua matawi ya benki hiyo katika Mkoa wa Iringa, Dodoma pamoja Njombe.

Bw. Enock amesema kuwa licha kufungua matawi hayo, wamefanikiwa kuongeza nguvu katika kukusanya madeni pamoja na kuboresha vitengo katika utendaji.

Amefafanua kuwa amana ya benki imekuwa kutoka shillingi bilioni 141 hadi kufika bilioni 149, huku katika upande wa mali (assets) imeongezeka kutoka bilioni 184 hadi kufikia bilioni 196.9.

Bw. Enock ameeleza kuwa wameweza kubana matumizi kutoka kutumia bilioni 5.9 na kupungua hadi kufikia bilioni 4.5.

"Tumepata faida ya bilioni 1.254 katika kipindi cha robo tatu ya mwaka" amesema Bw. Enock.

Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Mkombozi Profesa Marcellina Mvula Chijoriga, amesema kuwa wamejipanga kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja.

Prof. Chijoriga amesema kuwa lengo ni kuhakikisha wanatoa huduma bora ikiwemo kuongeza ada ya mapato yasiyokuwa na riba.

Hata hivyo amesema kuwa bodi imefanikiwa kushika nafasi ya tatu katika soko la hisa, na ushindi huo umetokana na ubora wa bodi katika utekelezaji wake.

"Benki ya mkombozi ni salama kwa mteja, nawakaribisha wateja kuwekeza" amesema Prof. Chijoriga.

Benki ya Mkombozi inamilikiwa na kanisani Katoliki kwa hisa za asilimia 46, na imekuwa na mipango mbalimbali katika kuhakikisha inaendelea kufanya vizuri.

No comments