Ads

Waziri Kabudi: JPM anamuenzi Hayati Mwalimu Julius Nyerere kwa Serikali kuhamia Dodoma na kutekeleza miradi ya maendeleo ya kimkakati


 

Hussein Ndubikile
Mwambawahabari
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamaganda Kabudi amesema Rais Dkt. John Magufuli anamuenzi Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere kwa kutekeleza adhma yake ya kuhamia Dodoma na kutekeleza miradi ya kimkakati ya maendeleo iliyoshindwa kutekelezwa kipindi chake kutokana na kukosekana fedha za utekelezaji.
Ameysema hayo jijini Dar es Salaam katika Kongamano la Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere lililoandaliwa na Kigoda cha Kiprofesa cha Mwalimu Nyerere cha Taaluma za Umaujumui wa Afrika pamoja kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm) pamoja  na Taasisi ya Uongozi.
Alisema tangu Rais Magufufuli aingie madarakani na miaka 20 baada ya Nyerere kufariki amekemea na kuishi katika misingi ya mwasisi huyo wa taifa ikiwemo kusimamia umoja, mshikamano uzalendo huku akisisitiza ametekeleza miradi ya ujenzi wa reli ya kisasa, ujenzi wa daraja la Ubungo pamoja na ujenzi wa Bwawa la kuzalisha umeme la Stiglers Gorge liliopo Rufiji wenye uwezo wa kuzalisha megawatt 2,115.
“ Rais Magufuli ametekeleza adhma yake ametekeleza miradi iliyomshinda mwalimu sababu ya ukosefu wa fedha amedhubutu Serikali kuhamia Dodoma ambapo kipindi hicho ilishindikana miradi migi ya maendeleo imetekelezwa, ’’alisema Profesa Kabudi.
Alibainisha kuwa Rais Dkt. Magufuli ametekeleza kwa vitendo sera ya Mwalimu Nyerere ya kuboresha miundo mbinu ya huduma za afya na kutoa elimu kuanzia elimu ya awali hadi kidato cha nne ambapo kila mwezi hutoa Sh bilioni 23.28 za elimu bure.
Alisisitiza kuwa miradi yote ya kimkakati imetekelezwa kwa fedha za wananchi na kwamba Rais Magufuli ametekeleza uboreshaji miundo mbinu ya afya kwa kujenga vituo vya afya 352 vilivyogharimu Sh mil 500 na Hospitali za wilaya 67.

Alifafanua kuwa katika kuhakikisha nchi inakuwa na umeme wa uhakika Serikali ina mpango wa kuongeza mabwawa mawili mkoani Njombe na kubainisha hata kipindi Mwalimu Nyerere huduma za afya na elimu zilikuwa ila kutokana na kusalitiwa na Shirika la Fedha Duniani(IMF) na Benki ya Dunia (WB) ililazimu Serikali kuleta mfumo wa kuchangia huduma hizo.
Pia amesema Rais Magufuli anatekeleza miradi hiyo lengo likiwa kuifanya nchi kuwa na uchumi imara, endelevu na kujitegemea na kwamba hata ulinzi wa rasilimali  za nchi umesimamiwa ikiwemo uzinduzi wa rada tano, marekebisho ya sheria ya madini ya mwaka 2010, maboresho ya mikataba kati ya Serikali na kampuni za TICTS na Airtel ambayo yote imekamilika.
Amekikumbusha chuo hicho kuienzi Lugha ya Kiswahili ili iendelee kutambulika na kuenea duniani na kusisitiza kama Serikali ilivyofanya jitihada lugha hiyo kuwa ya mawasiliano katika Vikao vya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).
Katika hatua nyingine, Waziri Kabudi alisema atakapomaliza ungwe ya uongozi atarudi chuoni hapo kuendele kukitumia kamwe hatakidharau kwani ndio kimemfikisha alipo na kuwaambia wanatalaamu wa Kemia wajiandae kwani hata Rais Magufuli amepanga kurudi chuoni baada ya kumaliza madaraka yake.
Kwa upande Makamu Mkuu Mstaafu wa Udsm ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kigoda hicho Profesa Rwekaza Mukandala alisema Mwalimu Nyerere alikuwa chachu ya kuanzishwa Udsm na kusisitiza kuwa alikemea mbwembwe, madai ya mishahara mikubwa na kutundika vyeti ukutani.
Naye Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa William Anangisye alisema wataweka orodha ya watu waliofanikisha kuanzisha chuo hicho ili kilichopo na kijacho kitambue mchango wao.
Profesa Anangisye alisema Mwalimu Nyerere alikuwa na utaratibu wa kwenda chuoni hapo kuzungumza na wanataaluma mambo ya kisiasa, kijamii na kiuchumi na kwamba Udsm inaunga mkono jitihada za Rais Magufuli za kuifikisha nchi kwenye uchumi wa kati kupitia uchumi wa viwanda pamoja na kuendelea kuwaamini wasomi katika uongozi.
Naibu Makamu Mkuu wa Taaluma wa Chuo hicho, Profesa Boniventure Rutinwa alisema chuo kinaendelea adma na sera ya nchi kukienzi na kukieneza Kiswahili kwa kuwavutia wageni kutoka nje ya nchi kuja kujifunza chuoni hapo.

No comments