CCM ILALA YAWAPA ONYO WAGOMBEA WATAKAO TUMIA RUSHWA SERIKALI ZA MTAA
NA HERI SHAABAN
CHAMA cha Mapinduzi CCM wilaya ya Ilala kimewapa onyo wagombea wa Serikali za Mitaa watakao tumia rushwa katika uchaguzi watashughulikiwa.
Tamko hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM wilaya Ilala Ubaya Chuma wakati wa hafla ya kuwaaga Wenyeviti wa Serikali za Mitaa wa halmashauri ya Ilala waliomaliza muda wao Octoba 06 mwaka huu ,hafla iliyoandaliwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Wilaya hiyo.
"katika Wilaya yangu ya Ilala tunataka viongozi bora ambao watatumikia wananchi sio bora kiongozi na watakao tumia rushwa wote watashughulikiwa "alisema Ubaya .
Ubaya aliwataka wana ccm wajipime wakiona wanatosha wachukue fomu za kugombea uongozi ila wasitumie rushwa.
Alishauri wale wenyeviti walio maĺiza muda wao kama wana endelea wawe wa kwanza kuchukua fomu za kutetea kiti hicho cha Mtaa.
Aliwataka washukuru Mwenyezi Mungu kwa kipindi walichokaa madarakani kuwatumikia wananchi vizuri wajipange kwa ajili ya kutetea nafasi hiyo kwa ajili ya kupeperusha bendera ya Chama cha Mapinduzi CCM .
Aidha aliwataka wajishushe kwa wananchi wote watakaopata ridhaa majina yao kurudi ili waweze kupita waje kushirikiana na Serikali kuwahudumia wananchi wa mitaa yao.
Alisema chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Ilala kimejipanga vizuri kushinda mitaa yote kitasimamisha wagombea wenye sifa.
Kwa upande wake aliyekuwa Katibu wa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Mariam Machicha ameomba Serikali kuwafikilia Wenyeviti wa Mtaa wakimaliza muda wao walipwe kama sehemu ya kiinua Mgongo kama wanavyolipwa madiwani na wabunge .
Naye Naibu Meya wa Halmashauri ya Ilala Ojambi Masaburi akijibu risala ya Wenyeviti kuhusiana na kupewa kinua mgongo alisema amezipokea atafikisha ngazi za juu ili yaweze kufanyiwa kazi ikiwemo katika baraza la madiwani la Manispaa ya Ilala .
MWISHO
Post a Comment