Ads

Serikali yaiagiza NACTE kuvichukulia hatua vyuo vinavyokiuka sheria, kanuni na taratibu katika kutekeleza wajibu wao

Image result for PICHA ZA OLE NASHA
Na  Hussein Ndubikile,
 Mwambawahabari
Serikali imeliagiza Baraza la Elimu ya Ufundi Nchini (NACTE) kuvichukulia hatua kali za kisheria vyuo vyote vilivyo chini ya baraza hilo vinavyokwenda kinyume  na matakwa ya sheria, kanuni  na taratibu ikiwemo kuchelewesha kuwasilisha matokeo, majina ya wanafunzi waliohitimu, kusajili wanafunzi wasio na sifa huku ikibainisha ukiukwaju huo husababisha wanafunzi kushindwa kuendelea na ngazi nyingine za masomo pamoja na kushindwa kupata vyeti kwa muda muafaka.

Aidha, imeliagiza baraza hilo kuhakikisha wanafunzi waliomaliza muda mrefu wanashughulikiwa ili wapate usajili ndipo ishughulikie wanafunzi wapya katika mfumo wa usajili unaotumiwa na baraza hilo (AVN)
 Maagizo hayo yametolewa jijini Dares Salaam  na  Naibu Waziri  wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha wakati wa ziara yake  ya kikazi ya siku mbili katika taasisi za zilizo zilizo chini ya wizara hiyo  ikiwemo NACTE , Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimuya Juu (HELSB) akiwa alieleza kukerwa na uwepo wa malalamiko mengi dhidi ya baraza hilo ambayo kimsingi chimbuko lake ni vyuo kukiuka masharti  ya kudahili wanafunzi nje ya mfumo unaosimamiwa na NACTE.

Malalamiko mengine ni vyuo kuchelewesha kuwasilisha matokeo ya mitihani ya wanafunzi NACTE kusababisha kuchelewesha wahitimu wengi kupata Hatizao za Matokeo (transcripts), NambayauhakikiwaTuzo (AVN) na Vyeti vya uhitimu.
Naibu Waziri Nasha alisema NACTE inatakiwa kuvichulia hatua vyuo vyote vinavyochelewa matokeo ya wanafunzi kwa kuvifutia udahili huku akibainisha vyuo vya binafsi na umma vitakavyobainikia kuwafanyia udahili wanafunzi wasio na sifa vifutiwe usajili wake.
Alibainisha kuwa  vipo vyuo vya Serikali vinavyolalamikiwa kwa matatizo sugu ya kushindwa kuwasilisha matokeo ya wanafunzi wahitimu hali inayochangia wanafunzi kushindwa kujiunga na ngazi nyingine za masomo ikiwemo Astashahada na Shahada huku akisisitiza kuwa vipo vyuo vinavyotumia udanganyifu kuwasajili wanafunzi wasio na sifa wakati vikitambua hilo ni kosa kisheria  NACTE ivifutie usajili wake kuondoa mkanganyiko unaotokea baada ya wanafunzi kuhitimu ikiwemo kushindwa kupata vyeti vya kuhitimu masomo yao.
Aliongeza kuwa udahili wanafunzi wasio na sifa katika ngazi zote husabababisha kupata wahitimu wasio na sifa katika soko la ajira pamoja na kuharibu mfumo wa elimu ya nchi na kwamba NACTE inatakiwa kuvichukulia vyuo vinavyofanya hivyo.
Pia aliiagiza idara ya mitaala ya NACTE kuandaa utaratibu kubadilsha mitaala ya masomo itakayoendana na mahitaji ya soko la ajira na karne 21 ya sayansi na teknolojia.
Katika hatua nyingine Naibu waziri Ole Nashaa mepongezamfumowamtandaowa NACTE ambao umeundwa na Taasisi hiyo ckushughulikia mifumo mbalimbali ukiwemo ulewa udahili ambao unahakiki taarifa za matokeo ya kila muhula ya mwanafunzi hadi anapomaliza taalumaa liyosomana kumthibitisha kwa ngazi inayofuata. Aidha, mfumo huo una hakiki matokeo yaliyotoka nje ya mfumo huo ili kumwezesha mwombaji  wa masomo ngazi ya chou kikuu kuweza kuendelea na masomo yake.
Naye Katibu Mkuu Mtendaji wa Shirikisho la Vyuo Vikuu Nchini (Tahliso), Alex Stepahno alisema wakati mwingine ucheleweshaji wa matokeo ya wanafunzi hufanywa na vyuo na kwa uzembe wa wanafunzi na kuiomba Nacte kuchukua hatua kali za kisheria kwa vyuo.
Aliliomba baraza hilo kuzungumza na wakuu wa vyuo suala la rushwa ya ngono vyuoni ili suala hilo lichukuliwe hatua na kusisitiza kuwa Tahliso itaendelea kushirikiana na NACTE na Serikali lengo likiwa kujenga taifa imara.

No comments