Ads

RC MAKONDA AZINDUA MFUMO WA KUWEZESHA WANANCHI KUTOA MALALAMIKO DHIDI YA WATENDAJI WASIOTEKELEZA MAJUKUMU YAO KWA KUTUMIA SIMU ZA MKONONI


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Paul Makonda* leo October 09 amezindua *Mfumo* wa kuwawezesha wananchi wa Mkoa huo kuwasilisha *kero na changamoto* walizonazo kwa kutumia *simu ya mkononi au Computer* na ujumbe wao kuwafikia watendaji kwa *haraka* na kupatiwa *majibu ndani ya muda mfupi* jambo litakalosaidia *kuokoa Muda na gharama za usafiri.*

*RC Makonda* amesema ameamua kuanzisha mfumo huo baada ya kubaini kuwa *wananchi wengi wamekuwa wakifika kwenye ofisi za umma* na kupewa majibu ya *"Njoo Kesho"* pasipokujua kuwa wamepoteza *muda na nauli* zao kufuata huduma.

Aidha *RC Makonda* amebainisha kuwa mfumo huo utakuwa ukipokea *taarifa* za malalamiko ya Watendaji wasiowajibika kuanzia *ngazi ya Mtaa, Kata, Wilaya hadi Mkoa* na taarifa zitawafikia Viongozi wote kuanzia *RC Makonda mwenyewe, Mkuu wa Wilaya husika, Mkurugenzi, Katibu tawala na Mkuu wa idara.*

Hata *RC Makonda* amewahimiza wananchi kutumia mfumo huo *kueleza kero zote zinazowakabili ikiwemo Afya, Barabara, Elimu, Maji, Umeme, Miradi inayokwama* pamoja na kutoa taarifa pindi wanapobaini *uhalifu kwenye mtaa.*

*Jinsi kuwasilisha ujumbe andika neno DSM kisha eleza changamoto zako kisha tuma kwenye namba 11000 au ingia kwenye Website www.malalamiko.dsm.go.tz na ujumbe wako utapokelewa mara moja na kupewa mrejesho.

No comments