DKT. SHEIN: SERIKALI ITAENDELEA KUWATUNZA WAZEE.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, ambaye pia, ni Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuwatunza na kuwaenzi wazee.
Dk. Shein aliyasema hayo leo Oktoba 9.2019 Mkoa wa Kusini Pemba wakati alipofanya mkutano na Wazee wa CCM wa Wilaya ya Chake Chake.
Rais Dk. Shein amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inathamini na inazijali juhudi za wazee walizozichukua hadi kupelekea kupatikana uhuru wa Tanganyika na uhuru wa Zanzibar kupitia vyama vya ASP na TANU.
Rais Dk. Shein amesema kuwa wazee ndio walioijenga Zanzibar na kuleta ukombozi na kuwakomboa wanyonge.
Post a Comment