Ads

MAADHIMISHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI KITAIFA 2019 KUFANYIKA MKOANI SINGIDA


Na Dotto Mwaibale, Singida

MAADHIMISHO ya Siku ya Chakula Duniani Kitaifa yanatarajiwa
kufanyika mkoani Singida ambapo Tanzania itaungana na nchi wanachama wa Shirika la
Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) katika kusherehekea siku hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana Mkuu wa
Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi alisema mgeni rasmi katika maadhimisho hayo
anatarajiwa kuwa Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga na kuwa yatazinduliwa kesho katika Uwanja wa Bombadia.
” Ndugu Wananchi napenda kuwafahamisha kuwa mkoa wetu
wa Singida umepewa heshima na Taifa kuwa mwenyeji wa Siku ya Chakula
Duniani.Maadhimisho haya yatazinduliwa kesho Oktoba 10, 2019 natoa wito kwa
wananchi wa Singida na mikoa jirani kujitokeza kwa wingi kwenye Uwanja wa
Bombadia ambako maadhimisho hayo yatafanyika kuanzia kesho na kufikia kilele
chake Oktoba 16, 2019.

Dkt. Nchimbi alisema kaulimbiu ya maadhimisho hayo  inasema “Lishe Bora kwa Ulimwengu Usio na Njaa” na kuwa kauli mbiu
hiyo inalenga kuhamasisha jamii na wadau wote wa sekta kilimo kuchangia katika
kuhakikisha nchi na dunia inakuwa na chakula cha kutosha wakati wote.
Alisema Takwimu za Wizara ya Kilimo zinaonyesha hali ya
upatikanaji chakula mwaka 2019/2020 ni nzuri, kwani nchi, ina chakula cha
kutosha. Kiwango cha utoshelevu wa chakula ni asilimia 119. Uzalishaji wa mazao
ya chakula ulifikia tani 16,408,309 ukilinganisha na mahitaji ambayo ni
tani  13,842,536. Kati ya hizo Tani
9,007,909 ni mazao ya nafaka na tani 7,400,400 ni mazao yasiyo
nafaka.Tunawapongeza watanzania kwa kutekeleza kauli mbiu hii kwa vitendo.

No comments