Ads

TAASISI YA FAHARI YAMUENZI NYERERE KWA KUPANDA MITI

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Viwege wilayani Ilala leo Octoba 14/2019 wamepokea msaada wa miti kwa ajili ya kupanda shuleni kwao,miti iliyotolewa na Taasisi ya Fahari Tuamke Maendeleo katika kumbukizi ya Mwalimu Julius Nyerere.

NA HERI SHAABAN
TAASISI ya Fahari Tuamke Maendeleo leo wamemuenzi Mwalimu Julius Nyerere kwa kupanda miti shule ya Msingi Viwege wilayani Ilala.

Miti hiyo ilitolewa na taasisi ya Fahari  Tuamke Maendeleo ilipandwa na Wanafunzi wa Shule  ya Viwege kwa kushirikiana na watumishi wa Fahari.

Akizungumza na waandishi wa habari  shule ya Viwege Mkurugenzi wa Fahari Tuamke Maendeleo  Neema Mchau alisema katika kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere  taasisi yake kwa kushirikiana na watumushi wake  wanaunga mkono Juhudi za Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwa vitendo.

"Taasisi ya fahari leo tumeungana Watanzania  katika kumbukizi ya Mwalimu Nyerere tumefanya usafi shule ya Msingi Viwege ,tumepanda miti pamoja na kutoa msaada wa vyakula na nguo kwa wanafunzi wenyeviti wenye mahitaji maalum yote ni sehemu ya mshikamano kwa kumuenzi mwalimu" alisema Neema

Neema alisema dhumuni la taasisi ya fahari kusaidia jamii ndani ya wilaya ya Ilala  pia kuwawezesha vijana wajitegeme na kuacha maisha tegemezi  .

Alisema katika mafanikio ya taasisi ya Fahari wamefanikiwa kuunda timu ya mpira wa miguu ambayo ilishiriki mashindano ya Vijana ya wilaya ya  Ilala na kupiga vita vijana wasijiusishe na dawa za kulevya.

Amewataka jamii kuiga misingi ya Mwalimu Julius Nyerere  kwa kusomesha watoto ili Taifa liwe bora watu wake wanatakiwa wapate elimu.

Amewataka wazazi kufatilia maendeleo ya watoto wao ya shule kila wakati kufanya ukaguzi wa daftari wakati wakitoka shule.

Kwa upnde wake Mwalimu Lucy Emanuel wa Shule ya Viwege ya watoto wa Mahitaji maalum alisema shule hiyo ina wanafunzi 26 wasichana 15 wavulana 16 ameipongeza halmashauri ya Ilala kuanzisha kitengo hicho katika shule hiyo  .

Mwisho

No comments