Ads

CTI Kuwatangaza washindi wa PMAYA Oktoba 17

Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Shirika la Viwanda Tanzania (CTI) linatarajia kuwatangaza washindi wa tuzo za Rais za Wazalishaji Bora Viwanda (PMAYA) siku ya Oktoba 17 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Washindi wa tuzo hizo za mwaka 2018 zimelenga kutoa fursa kwa makampuni kuonyesha ufanisi katika uzalishaji, kutangaza bidhaa pamoja na kuongeza ubora wa bidhaa na huduma.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Viwanda Tanzania (CTI) Bw. Leodegar Tenga, amesema kuwa maandalizi ya shindano yamekamilika.

"Nawaomba wanachama pamoja wamiliki wa viwanda kushiriki katika hafla ya kuwatangaza washindi" amesema Bw. Tenga.

Bw. Tenga ameeleza kuwa tukio la PMAYA linatambulika na CTI kama muhimu wa sekta ya viwanda nchini katika kutambua jukumu na mchango wao katika sekta ya viwanda, uchumi pamoja na kuwavutia wawekezaji.

Amefafanua kuwa kutangaza umuhimu wa sekta ya viwanda nchini itasaidia kuongeza ubora katika shughuli za uzalishaji pamoja na kukuza biashara nchini.

Katika hatua nyengine amewashukuru benki ya CRDB kuwa wadhamini wakuu wa PMAYA katika kufanikisha kila jambo linakwenda sawa.

Hata hivyo amewataja wadhamini wengine ambao ni Motisun, PanAfrican Energy, ALAF Limited, Dar es Salaam Serena hotel, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Giz Creating Perspective na montage.

No comments