Ads

Wadau wa Kavazi Mwalimu Nyerere wakutana kujadili Maendeleo Afrika.

Mkurugenzi wa Kavazi Mwalimu Nyerere, Prof. Issa Shivji.
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Watanzania wametakiwa kuwa wazalendo katika utekelezaji wa majukumu ikiwemo kuwa na umoja pamoja kuchukia rushwa,  jambo ambalo litasaidia kupiga hatua taifa la Tanzania.

Wakizungumza wadau mbalimbali leo jijini Dar es Salaam wakati wakichangia mada ya 'Toward feminist Pan-Africanism and Pan- African Feminism' uliongozwa na Mkurugenzi wa Kavazi Mwalimu Nyerere, Prof. Issa Shivji, huku mtoa mada akiwa Prof. Sylvia Tamale kutoka Chuo Kikuu cha Makerere.

Wadau hao wamesema kuwa ili kufika malengo nchi za afrika zinatakiwa kuwa na umoja katika kufata utamaduni wao na kuacha kuiga utamaduni wa kigeni.

Mshiriki wa majadala huo Bw. Innocent John, amesema kuwa kuna changamoto katika nchi za afrika hasa kwa viongozi katika utekelezaji wa majukumu yao.

Ameeleza kuwa baadhi ya viongozi wamekuwa hawafati katiba za nchi zao jambo ambalo ni kikwazo katika kufika malengo.

Naye Bw. Stanslaus Emmanuel, amesema kuwa umoja katika nchi za afrika kwa vijana umeondoka kwa mazingira ya sasa.

Ameeleza kuwa ni vizuri elimu inatakiwa kutolewa kwa vijana kuanzia elimu ya msingi na kuendelea ili kumkumbuka mwalimu nyerere.

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (UDSM) Twebaze Phionah, amesema kuwa  jambo la msingi tunapaswa kuacha kuendeleza mila zetu, jambo ambalo litasaidia kusonga mbele.

"Hatupaswi kujibadilisha kwa kuiga utamaduni watu wengine" amesema Phionah.

Kwa upande wake Prof. Shivji amewataka vijana kuendelea kupambana ili kuleta mabadiliko katika kupigania nchi za afrika.

Ameeleza kuwa tunatakiwa kuacha kuingia katika udini na ukabila kwani sio rafiki katika nchi za afrika.

Awali akitoa mada Prof. Tamale, ameeleza kuwa ni vizuri kuelewa mfumo wa nchi za afrika kitu ambacho kitatusaidia katika utekelezaji.

"Changamoto kubwa afrika watu wengi hawana uwelewa wa mfumo ulivyo" amesema Prof. Tamale.

No comments