DC MJEMA AHIMIZA MIRADI YA KIMKAKATI KUKAMILIKA KWA WAKATI.
Na John Luhende
Mwamba wa habari
Mkuu wa wa wilya ya Ilala Mhe Sophia Mjema ,amewataka
wakandarasi wanaojenga miradi ya kimkakati kufanya kazi usiku na mchana
ili waweze kukamilisha
ujenzi kwa wakati .
Dc Mjema ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake
kutembelea na kukagua maendeleo ya
ujenzi huo katika ujenzi wa soko la kisasa kisutu , ujenzi wa machinjio Vingunguti ,ujenzi wa mabweni shule ya
sekondari Jangwani ambapo alisema
katika kuhakikisha kazi inafanyika bila kusimama ofisi yake imeweka watu
kila mradi watakao kuwa wana simamia na kumpataarifa marakwamara.
Aidha akikagua ujenzi katika hospital ya
Wilaya Kivule,Mjema alitoa agizo
kwa mkurugenzi kuhakikisha
anapeleka vifaa vya ujenzi kwa
wakati .
“Nimefika hapa katika ujenzi wa hospitali sijafurahishwa kukuta kazi imesimama kisa Cement imeisha ,na
maelezo niliyopewa inaonekana mkurugenzi amechelewesha malipo hali halikubaliki namtaka mkurugenzi asisubiri vifaa vya ujenzi
kuisha ndipo afanye manunuzi majengo
haya nataka mpaka tarehe 30 yawe yamakamilika “Alisema Mjema .
Kwa upande wake msimamizi wa
mradi wa ujenzi wa soko la kisutu Mvungi Ismail, alisema ujenzi wa soko hilo ulichelewa kuanza kwakuwa
kulikuwa na changamoto ya udongo katika eneo la ujenzi lakini sa imetatuliwa na
ujenzi unaendelea umefikia asiliamia 5%, na jingo hilo sasa litakuwa imara
bilashaka.
Naye msimimamizi wa ujenzi wa machinjio ya kisasa Vingunguti Elisante Uromi kutoka shirika
la nyumba( NHC ), alisema
wanafanyakazi usiku na mchana kuhakikisha wanamaliza kazi hiyo kwa
wakati sawa sawa na agizo la serikali
Katika hatua nyingine DC Mjema ametembelea shule ya
sekondari Pugu na kuagiza kukomeshwa kwa tabia ya uvamizi wa eneo la shule hiyo.
“Uvamizi huu umefanywa na watoto wa waliokuwa watumishi
wa wazungu wao wanadaikuwa wamerithishwa na wazazi zao na mababu zao lakini ukweli nikwamba hayo siyo maeneo
yao yalikuwa na maeneo ya serikali tuna fuatilia na mikataba ipo tutahakisha
maeneo ya serikali yanalindwa nataoa
wito kwa wote wanaokalia maeneo haya kuyaachia
na viongozi wa ngazi za mitaa naomba wayalinde maeneo haya”Alisema.
Jovinus Mutabuzi , ambaye ni mkuu wa shule ya sekondari
Pugu alisema shule hiyo imeathirika na uvamizi huo ,kwani
watu wamekaribia eneo karibu na shue wengine wamejenga baa wanapiga mziki
wanavurugu utulivu wa wanafunzi katika masomo .
‘’Maeneo ya shule yatengwe na makazi
kama walimu pia tunapata changamoto wanafunzi wanavutika na mabo
yanayofanyika mtaani tunakuwa na kazi ya ziada kuwalinda wanafunzi kwani shule
yetu haina hata uzio tunashukuru taarifa
zimemfikia mkuu wetu wa wilaya tuna matumaini mgoro huu utakwisha”Alisema Mkuu wa shule.
Hatata hivyo mkuu huyo aliiomba serikali kuipekea maji
shule hiyo ili kuondokana na adha ya ukosefu wamaji kwa wanafunzi na walimu .
Post a Comment