Ads

Maisha Njema Foundation, Bilal Muslim Mission yaendesha kambi ya huduma za afya bure kwa watu 1311



Hussein Ndubikile, 
Mwambawahabari
Taasisi ya Maisha Njema kwa kushirikiana na Jumuiya ya Bilal Muslim Mission ya Dar es Salaam imeendesha kambi ya huduma za afya ya bure kwa kutoa matibabu ya watu 1,311 huku lego likiwa kuwafikia watu 2,000.
Kambi hiyo ya siku imejumuisha upimaji na utoaji matibabu bure kwa watu walliobainikia kuwa na magonjwa ya macho, meno, presha na sukari.
Akizungumza katika kambi hiyo iliyowekwa wilayani Temeke Msimamizi wa kambi hiyo Daktari Dayyanah Karim alisema siku ya kwanza ya kambi hiyo takribani watu 300 walipatiwa matibabu na kwamba wanafunzi 50 wa Shule ya Bilal Comprehensive walikuwa wakisubiri matibabu.
“ Malengo yetu ni kuwafikia watu 2000 tunashukuru mwitikio ni mzuri watu wamejitokeza madaktari na wasaidizi wanafanya kazi kuhakikisha kila aliyekuja hapa anapimwa na kupatiwa matibabu,” alisma Daktari Dayyanah.
Alibainisha kuwa wagonjwa waliobainika kuwa na magonjwa ya macho ikiwemo presha ya macho walipatiwa miwani huku akisisitiza watu 50 waliokutwa na mtoto wa jicho watapelekwa Kibaha katika hospitali ya jumuiya hiyo.
Alifafanua kuwa  waliopatikana na magonjwa ya meno waling’olewa, kuzibwa na kusafishwa na kwamba wengine walipewa dawa ya kusafisha (Sensodyne).
Daktari Dayyanah alisema kambi hiyo madaktari na wasaidizi jumla ya 90 na kubainisha wanatoa huduma za afya bure kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo TRH, Kampuni ya Ulinzi ya G1, Mohamed Enterprises ltd, International Optica na Smile Dental Clinic, Hospitali ya  Mediwell na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH).
Pia alisema kambi hiyo ni ya sita kwa mwaka huu na mwaka kambi ya mwezi Disemba  huduma ya matibabu ya Saratani na magojwa ya sikio ikiwemo tatizo la usikivu ambapo kifaa cha usikivu kitatolewa bure.
Kwa upande wake Msimamizi Msaaidizi wa kambi hiyo, Ali Dharamsi alisema kambi hiyo imekwenda vizuri kwa wagonjwa kupatiwa matibabu na kwamba wataendelea kutoa huduma za afya bure.

No comments