Taasisi ya dini ya kiislam ya Khoja Shia kutibu macho bure
Mratibu wa kambi ya macho katika Taasisi ya
Khoja Shia Alirge Bandari akizungumza na wandishi wa habari Katika kambi ya
macho (kushoto) Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Kata ya Kisutu Al Hajj Mahmood
Amirali (PICHA NA HERI SHAABAN).
NA
HERI SHABAN, DAR ES SALAAM.
Taasisi ya dini ya kiislam ya Khoja Shia leo wamezindua kambi ya miezi miwili
ya uchunguzi wa macho bure kwa wananchi.
Uzinduzi
huo ulifanyika katika kambi hiyo ya KhojaShia Wilayani Ilala wanangalia
bure mtoto wa jicho kila jumamosi na Jumapili kwa muda wa miezi miwili.
Akizungumza
na waandishi wa habari Mratibu wa kambi hiyo Alirga Bandari , alisema dhumuni
la kambi hiyo kuimalisha afya za Watanzania ili tuwe na Taifa imara.
"Tumeanza
kambi ya macho mtu akibainika kama ana mtoto wa jicho anafanyiwa upasuaji
bure " alisema Bandari.
Bandari
alisema kwa Mkoa wa Dar es Salaam kambi ipo wilaya ya Ilala huduma inatolewa
kwa mwaka mara moja,pia katika mikoa ya Tanga ,mkoa Pwani Bagamoyo,Kigoma,
Lindi.
Aidha
alisema pia katika kambi hiyo wanangalia afya ya meno kwa siku za jumapili peke
yake huduma hiyo nayo ni bure.
Kwa
upande wake Daktari wa macho Mwaihojo Justune alisema toka huduma hiyo ya
kuwafanyia uchunguzi wa macho bure zaidi ya wananchi 10,000 wamepewa huduma
tayari na mafanikio makubwa.
Mwandishi wa habari Heri
Shaaban (kushoto) akiangaliwa macho na Dkt. Mwaihojo Justine katika kambi ya
Macho Taasisi ya Kiislam ya Khoja Shia huduma hiyo bure kwa wananchi kwa
muda wa miezi miwili Jumamosi na Jumapili (PICHA NA MWANDISHI WETU).
Mwaihojo
alisema kuna tatizo la presha ya macho wagonjwa wengi waligundulika na tatizo
hilo.
Alisema
wagonjwa wakigundulika wana tatizo wanapewa rufaa ya kwenda
Amana,Muhimbili,Temeke,Mwananyamala.
"Tatizo
la upofu wa macho ukishindwa kutibu mapema unapata upofu wa macho uwezi kupona
" alisema Mwaihojo.
Post a Comment