MBUNGE JUMAA AWATAKA WATENDAJI KUFICHUA WAHUJUMU UCHUMI
NA HERI SHAABAN
Mwambawahabari
MBUNGE wa Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa ,amewataka Watendaji,Wenyeviti kumsaidia Rais katika kuwafichua wahujumu uchumi.
Mbunge Juma aliyasema hayo Dar es Salaam leo wakati wa kuzungumza na waandishi wa habari kwa ajili ya kumpongeza Rais John Magufuli katika kutekekeza miradi ya maendeleo na kutoa msamaha kwa vigogo wahujumu uchumi .
"Natoa pongezi kwa Rais wa awamu ya tano kwa kusimamia nidhamu katika nchi yetu na kuibua miradi ya kisasa ya maendeleo ujenzi wa Reli ya kisasa,ujenzi wa miundombinu na kuongeza ndege mpya hivyo kila mtendaji anatakiwa kusimamia upande wake katika kumsaidia Rais wetu"alisema Jumaa.
Jumaa alisema katika juhudi za kumsaidia Rais kila Mtendaji anatakiwa kuwajibika katika sehemu yake ,Wabunge,Watendaji na Wenyeviti.
Aidha alisema kwa sasa Rais ametunganisha na kuwa wamoja nidhamu ipo kila sehemu uchumi umekuwa na viwanda vimeongezeka,sekta ya utalii pia imekuwa.
Aliwaka,watanzania kumsdia Rais katika Tanzania ya uchumi wa viwanda Rais Magufuli ni Rais wa mfano tumtumie vizuri watanzania na Afrika kwa ujumla.
Akielezea kukua kwa mapato halmashauri ya kibaha Vijijini alisema serikali ya awamu ya tano wameweza kusimamia mapato vizuri na kujenga masoko na vituo vya afya katika halmashauri hiyo.
Aliwataka watendaji wote kuwajibika katika kufanya kazi wasimbebeshe Rais mzigo kila mtu asimamie upande wake na kusimamia mapato ya nchi vizuri ili zipatikane fedha zipelekwe katika huduma za jamii ikiwemo afya .
Post a Comment