SERIKALI YAKABIDHI HATI YA KIWANJA ALICHO AHIDI RAIS MAGUFULI KWA TAASISI YA AL-HIKIMA FOUNDATION.
Na John Luhende
Mwamba wa habari
Serikali imeitaka taasis ya Al-hikma Foundation ,kulitumia kwa makusudi yaliyokusudiwa eneo walilopewa na serikali na kwamba Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli alitoa eneo hilo kwa immani ya kusaidia
katika maendeleo kwa jamii.
Hayo yamesemwa na waziri wa maliasili na utalii Mhe. Hamis
Kigwangala alipo mwakilisha Waziri mkuu
Kasim Majaliwa ,katika makabidhiano ya
hati ya kiwanja namba 118 Block E Temeke , kilicho tolewa na Rais Magufuli kwa
taasisihiyo ambapo walikiomba katika mashindo ya ya Afrika ya kusoma qurani
yaliyofanika uwanja wa taifa mwezi mei 2019.
Alisema serikali
serikali ilirdhia kutoa endeo hilo ambalo lilikuwa mali ya umma ili
taasisi hiyo ijenge Hospitali kama ilivyo omba hivyo alisema lisibadilishwe matumizi.
‘’Mheshimiwa waziri mkuu amenituma nisema kwamba Rais anamatarajio makubwa na taasisi hii , mali hii anayowapa mtaenda kuitendea haki katika eneo hili kwa
uaminifu wa hali yajuu tusimwangushe
kama mlivyo andaa mashindano ya
qurani kwa ustadi wa hali ya juu kadhalika hapa mfanye kitu kinacho endana na
hadhi hiyo “Alisema
Aidha Kigwangala
aliwataka wanafunzi wanao soma katika
shule za Alhikima na shule za umma kusoma kwa bidii , na
kuwataka wazazi kupeleka watoto wao katika shule hizo kwani zina matokeo mazuri napia aliwatawanafunzi pamoja na kusoma masomo ya dini kuto acha
kusoma elimu dunia kwani kila elimu inaumuhimu wake.
Aliwataka waislamu na
watanzania kumuungamkono na
kumuombea Rais Magufuli kwani anania ya
dhati kuiletea nchi maendeleo na wajitokeze kwa wingi katika uchaguzi wa
Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika
mwishoni mwa mwaka huu kuchagua viongozi waadilifu wenye mfano wa Magufuli.
Kwa upande wake Rais wa Taasisi hiyo Shekh
Sharifu Abdullkadri ,amemshukuru Rais
Magufuli kwa kutoa kiwanja hicho na kusema kuwa kila ijumaa wataendelea
kumuombea Rais Magufuli na kuiombea nchi kwa ujumla .
Naye Mkurugenzi wa Taasisi hiyo ambaye pia ni Mhadhiri wa
kamataifa Shekh Nourdin Kishik ,alisema
tangu wamepewa eneo hilo na Rais mwezi
mei na kwamba walichelewa kuifanya hafla
hii kwa kuwa walikuwa na majukumu mengi baada ya Ramadhani na baadaye kwenda
hija ,na kusema kuwa Taasisi hiyo
inabahati na Rais Magufuli kwa kuwa
alisha wahi kuwa saidi kipindi cha nyuma
walipo zungushwa kupata eneo hilo .
‘’Baada ya kuzungushwa sana eneo hili wakati akiwa waziri
wa Ardh na maba na maendeleo ya makazi
alituuliza kote mlikopita hamja ombwa rushwa na si tulimwambia hatukuombwa labda kama
tulitengenezewa mazingira hayo lakini hatukuambiwa wazi, kwa sisi Al- hikima ambao tuna mfahamu tangu 2007 ,baada ya siku
mbili wakati huo akatusaidia tuka pata usajili wa shule zetu na sasa ametupatia
kiwanja hiki tuna shukurusana hatuna cha kumlipa ila tuemuombea dua kubwa Mungu ampe wepesi katika mambo yake “Alisema
Awali akitoa salamu za
malezi wa taasisi hiyo kwa niaba ya Rais mstaa Ali Hassan Mwinyi ,Dkt
Hussein Al Hassan Mwinyi alimshukuru Rais
Magufuli kwa wema alioitendea taasisi hiyo na kupongeza taasisi hiyo kwa
kuendelea kuyafanya kuwa makubwa mashindano
ya quran na kutiza agizo la Mtume Muhama la kumlipa mtu aliye watendea
wema kwa kumuombea dua.
Post a Comment