MTANDAO WA TGNP YAENDESHA WARSHA KWA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU WANAWAKE NA UONGOZI
Mkurugenzi wa TGNP Mtandao Lilian Liundi
Mkurugenzi wa TGNP Mtandao Lilian Liundi amefungua warsha ya Waandishi wa habari ngazi ya jamii kuhusu wanawake na uongozi wanawake katika uongozi ili kuwajengea na kuwaongezea uelewa na uwezo waandishi hao wa habari namna ya kuripoti masuala ya kijinsia hasa katika kuhamasisha ushiriki wa wanawake na vijana kwenye uongozi.
Warsha hiyo ya siku tatu iliyofunguliwa Jumatatu Septemba 16,2019 inafanyika katika ukumbi wa TGNP Mtandao uliopo Mabibo Jijini Dar es salaam ikikutanisha waandishi wa habari 43 kutoka mikoa mitano ambayo ni Shinyanga,Simiyu,Kigoma,Tabora na Mara.
Akifungua warsha hiyo,Liundi amesema lengo kubwa ni kuwajengea uwezo waandishi wa habari juu ya kutoa taarifa zenye mrengo wa kijinsia hasa zenye kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika uongozi ikiwemo kubadili mitazamo na mila hasi zinazozuia ushiriki wa wanawake katika uongozi.
"Lengo la mradi huu unaotekelezwa na TGNP Mtandao kwa ushirikiano na UN Women ni kuongeza namba na ushiriki wa wanawake katika nafasi za uongozi kisiasa na ngazi mbalimbali za maamuzi.Waandishi wa habari mna nafasi kubwa sana ya kuhamasisha ushiriki wa wanawake na vijana kwenye uongozi. Naamini kupitia warsha hii ya siku tatu mtakuwa chachu ya mabadiliko katika kuhamasisha wanawake kushiriki katika nafasi za uongozi",amesema.
"Jinsia ni suala la kimaendeleo,hatuna budi kwa pamoja kutoa kipaumbele ili kuongeza ushiriki wa wanawake wenye tija katika maendeleo.Kwa mantiki hii TGNP Mtandao tumeamua kuandaa mafunzo haya kwa kutambua umuhimu wa vyombo vya habari katika kuelimisha,kubadili tabia na mitazamo ili kuongeza uelewa katika jamii juu ya dhana nzima ya uongozi kwa wanawake na umuhimu wa wanawake katika kushika nafasi za maamuzi",ameongeza Liundi.

Mkurugenzi wa TGNP Mtandao Lilian Liundi akifungua warsha ya Waandishi wa habari 43 kutoka Mikoa ya Shinyanga,Simiyu,Kigoma,Tabora na Mara kuhusu ushiriki wa wanawake katika uongozi, uliofanyika katika ukumbi wa TGNP Mtandao jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa TGNP Mtandao Lilian Liundi, akifungua warsha ya Waandishi wa habari kuhusu ushiriki wa wanawake katika uongozi katika ukumbi wa TGNP Mtandao jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa TGNP Mtandao Lilian Liundi, akifungua warsha ya Waandishi wa habari kuhusu ushiriki wa wanawake katika uongozi.
Mkurugenzi wa TGNP Mtandao Lilian Liundi, akifungua warsha ya Waandishi wa habari kuhusu ushiriki wa wanawake katika uongozi.
Afisa Habari wa TGNP Mtandao,Monica John akizungumza wakati wa warsha hiyo.
Mwezeshaji Beatrice Ezekiel akitoa mada kuhusu dhana mbalimbali za Jinsia ikiwemo 'Fikra Mgando'.
Waandishi wa habari,Frank Mshana kutoka Shinyanga na Happiness Severine kutoka Simiyu wakiwa ukumbini.
Waandishi wa habari wakiandika dondoo muhimu wakati wa warsha hiyo.
Washiriki wa warsha wakiwa ukumbini.
Warsha inaendelea.
Warsha inaendelea.
Post a Comment