Ads

Makonda awajia juu watendaji wakwamishaji miradi ya maedeleo ya kimkakati aunda kamati ya kuangalia mwenendo

Image result for PICHA ZA MAKONDA

Hussein Ndubikile, 
Mwambawahabari
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewakemea na kuwaonya watendaji wote wanaokwamisha Miradi ya Maendeleo ya Kimkakati  kwa kusema  wataobainika watachukuliwa hatua za kinidhamu na kuwajibishwa.

Aidha, Mkuu huyo amesema ataunda Kamati itayokuwa na jukumu la kuangalia mwenendo wa miradi yote ya kimkakati kwa kupokea taarifa kila baada ya wiki mbili ndani ya mwezi lengo likiwa kuwabaini wanaokwamisha wachukuliwe hatua.

Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya Rais John Magufuli kutembelea miradi hiyo ikiwemo ya Machinjio ya Vingunguti na Coco Beach na kukuta ujenzi ukiwa hauendelea licha ya Serikali kutoa fedha za ujenzi.

Hayo ameyasema jana katika Kikao cha kupokea msaada wa kusomesha watoto wa kike 100 wa kidato cha tano waliochaguliwa mwaka huu wanaochukua masomo ya Sayansi kutoka kwa Balozi wa Nchi za Falme za Kiarabu.

Alisema miradi yote ya kimkakati iliyokwama ujenzi inakwamisha na watendaji licha ya Serikali huku akibainisha alishakaa vikao na watendaji hao kujua mwelekeo wa miradi ila cha kushangaza pasipo sababu za msingi imesimama ujenzi hauendelei.
“ Nafanya vikao na watendaji wangu nawasisitiza waharakishe miradi ikamilike laikini wanashindwa kutekeleza Rais Magufuli amepita kuona maendeleo Machinjio ya Vingunguti amekuta hakuna kinachoendelea ni aibu,” alisema.

Makonda alisema watendaji wa mkoa huo wamemvua nguo na kwamba angekuwa haofii njaa angeshajiuzulu nafasi yake kwani haipendezi watu wazima kufanya kazi kwa kusukumwa.

Alibainisha kuwa miradi yote iliyokwama fedha zake ilishatolewa muda mrefu ukiwemo wa Machinjio ulipewa Sh billion 12.5 na Ufukwe wa Coco Sh bilioni 14 ila cha ajabu miradi hiyo imekwama licha watendaji kupewa maelekezo awali.

Alisisitiza kuwa wapo madiwani waliogombea nafasi kwa ajili ya kujinufaisha kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma na kwamba wanapoona mambo yao hayaendi wanakawamisha miradi.

Aliitaja miradi mingine inayokwamishwa ni Mradi wa Ujenzi wa Soko la Kisutu, Stendi ya Mabasi-Mbezi na wa Magomeni huku akiwasisitiza kuwapuuza wanasiasa wakwamishaji maendeleo.

Alifafanua kuwa kamati atakayounda itafuatilia miradi ya kimkakati mwenendo wake na kwamba watakaokuwamo wataleta taarifa za miradi hiyo kwa muda uliowekwa.
Aliongeza kuwa mradi wa Ufukwe wa Coco unavyozidi kuchelewa ndi mapato yanavyozidi kupotea na kuwataka Wakuu wa wilaya kuwa wakali kwenye maeneo yao miradi ikamilike kwa wakati.

Pia alisema ana mpango wa kupeleka pendekezo la kukabidhiwa miradi yote ya kimkakati ili kuachana na wanasiasa wanaokwamisha miradi hiyo lengo likiwa kuunga mkono juhudi za Rais  Magufuli za kuwaletea wananchi maendeleo.

No comments