Ads

KUMBILAMOTO AKABIDHI RUNINGA MPYA KWA WANACHAMA WA YANGA TAWI LA MTAMBANI -VINGUNGUTI.


Mwambawahabari
Msitahiki meya wa manispaa ya ilala Omary Kumbilamoto ameitaka klabu ya yanga alimaarufu kama klabu ya wananchi kuchezea mpira mguuni na sio mdomoni kama ambavyo imezoeleka kwa klabu nyingi hapa nchini.

Kumbilamoto ametoa Rai hiyo akiwa katika hafla fupi ya kukabidhi runinga katika tawi la yanga la mtaa wa mtambani kata ya vingunguti ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi yake kwa tawi hilo.


Wakifurahia ujio huo wa meya mwenyekiti wa tawi hilo Othmani   Yahaya amesema TV iliyokabidhiwa kwao ni ishara ya upendo na ushirikiano wa watanzania huku akielezea jinsi itakavyotumiwa kutazama michezo mbalimbali lkn pia kuifanya kama chanzo cha kipato kwa kuonesha mechi za ligi mbali mbali.

Mara baada ya wanachama wa tawi hilo kupokea runinga hiyo ikawa ni fursa kwao kushukuru huku wakicheza kwa bashasha kigoma chenye asili ya kabila la wazaramo.

Katika hafla iyo meya huyo pia ameambatana na msemaji wa Ruvu shooting masau bwire ambaye amesisitiza kuwa ule mpapaso walioupata yanga uwe funzo katika kujipanga katika mechi wao dhidi ya zesco ya  Zambia.


No comments