Ads

BRELA ya toa mafunzo Manispaa ya Ilala kuhusu mfumompya wa Ukataji leseni za biashara.




Na John Luhende 
Mwambawahabari 
Katika  kuwajengea uwezo watumishi wa halmashauri wanaohusika na utoaji wa leseni za biashara  Wakala wa usajili wa leseni na  biashara  hapa nchini  Brela,   imeendelea kufanyamafunzo  kwa maofisa wa Tehama  ili waweze kutoa huduma kwa njia ya mfumo unaofahamika kama  mfumo  wa dirisha la  taifa la biashara .
Akizungumza katika mafunzo hayo Mkurugenzi wa leseni wa wakala wa leseni na biashara  Adrew   Mkapa, alisema  mafunzo hayo yataendeshwa katika wilaya sita hapa nchini kama mfano na kwamba  mafunzo hayo yatawajengea  uwezo watumishi kabla ya kuanza kutumika rasmi kwa mfumo huo.
“Leseni za biashara ziko katika makundi  mawili kuna kundi A  hizi zilikuwa zinatolewa na wiazra ya viwanda na biashara  na baadaye kuanzia mwaka 2017 zilhamishiwa Brela na zikawa zimekuja na mradi wa mfumo  wa  dirisha la  taifa la biashara ambao unapande mbili ,moja kutoa taarifa za kibiasha ,mbili kuomba na kutoa leseni kwanjia ya tehama”Alisema 
Lesen kundi B , hutolewa na halmashauri,miji na majiji serikali iliamua hizi nazo zitolewa kwa njia ya mfumo wa tehema na kwa kuanzia zimeteuliwa wilaya sita kote nchini kwaajili ya majaribio na baadaye utatekelezwa nchi nzima ,baadhi ya wilaya zilizopendekezwa kwa majaribio hayo ni pamoja na Ilala ,Chalinze ,mafinga , Bukoba , karagwe na  Mwanza .
Alisema baada ya mafunzo haya kikosi kazi kimeundwa kufuatilia mrejesho na baaye mfumo huu utatumika nchi nzima hakutakuwa na maombi ya leseni tena kwa mfuma wa zamani bali wataomba kupitia mtandoa .
Tawi Godfrey Kihomile , meneja wa mradi huo alisema   kuanza kutolewa kwa mafunzo hayo nihatua za utekelezaji wa mpango wa serikali ya awamu ya tano katika kuelekea Tanzania ya uchumi wakati.
“Hatuwezi kufikia  uchumi wakati bila kutengeneza au kuwa na mfumo wezeshi kwa wafanyabiashara na walipa kodi ,mfumo huu utaongeza uchumi kwa maana ya makusanyo ya kodi na kuwapunguzia wafanya biasha usumbufu na upotevu wa muda kufuatilia leseni  hivyo muda huo sasa watautumia katika uzalishaji mali  pia utondoa mzigo kwa watumishi “Alisema .
Kwa upande wake afisa biashara wa Manispaa ya Ilala Nikas Msemwa, alisema mafunzo hayo wameya pokea kwa mwitikio chanya kwani ni mfumo mzuri ambao umelenga kuwapunguzia usumbufu watumishi na wafanya biashara pia utapunguza gharama za uendeshaji wa ofisi. 

No comments