Kamati ya Viongozi wa Dini Mbalimbali kuwapa mafunzo wanawake 100 kushiriki kugombea uongozi
Hussein Ndubikile. Mwambawahabari
Kamati ya Viongozi wa Dini Mbalimbali imeandaa mafunzo kwa wakinamama 100 yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kushiriki kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.
Mafunzo hayo ya siku mbili yaliyopewa kauli mbiu ' Wanawake na Uongozi wa Kuchaguliwa' yatafanyika kuanzia septemba 4 hadi 5 itakayokuwa kilele chake.
Hayo yalibainishwa jana jijini Dar es salaam na Katibu wa Baraza Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Padri Charles Kitima viongozi wa dini wameamua kufanya mafunzo hayo baada ya kubaini wakinamama wengi hawashiriki katika kugombea nafasi za uongozi kutokana na kutojengewa uwezo.
Alisema kuwa wamebaini wakinamama ni watu wa kujitoa kwa jambo lolote hivyo wao kama viongozi wa dini wameliona hilo na kuwahamasisha kushiriki mafunzo hayo.
"Tanzania tuna rasilimali nyingi za kuwawezesha watu kupata maendeleo ambapo tumeona makundi ya akinamama wakijtoa kwenye kuziendea fursa hizo hivyo sisi viongozi wa dini tumeliona ni kundi linalohitaji kujengewa uwezo katika masuala kisiasa,kiuchumi na kijamii ," alisema Kitima
Kitima alisema kuwa wanawake wakipewa mbinu za kitaalamu wanaweza kuchangia kupunguza changamoto mbalimbali zinazolikabili jamii hususan kwenye masuala ya malezi kwa watoto na vijana ,kwenye masuala ya afya na shughuli za ujasiliamari.
Aidha kwa kipindi kirefu kulikuwa na harakati za kujikomboa kwao kutoka kwenye mfumo dume ambapo walipaza sauti zao zilizoweza kusikika na baadhi ya viongozi wetu.
Hata hivyo akinamama kwa asilima kubwa wameweza kuonesha jitihada mbalimbali za kuliletea taifa maendeleo kupitia vikundi vya utoaji hamasa na kutoa misaada kwenye makundi yenye uhitaji pamoja na kushiriki kwenye zoezi la uandikishwaji na upigaji wa kura.
Kiongozi huyo alifafanua kuwa kupitia mifano ya viongozi wanawake ambao waliweza ama wameonesha umahiri mkubwa katika kuliongoza jahazi la nchi hii kwenye kuzitendea haki nafasi zao za uongozi.
Pia alisema mafunzo hayo yatawajengea ujasiri wanawake washiriki kuhamasisha wenzao kujitokeza kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kuwaaminisha wananchi kuwa wana uwezo kuiongoza jamii.
Padri Kitima aliatabaisha kuwa kutokana na wanawake kunyimwa uwezo wa kugombea nafasi za uongozi kumechangia kwa kiasi kikubwa kukosekana viongozi vielezezo akiwatolea mfano Asha Rose Migiro na Getrude Mongella.
Aliongeza kuwa mafunzo hayo yatasaidia wanawake kushiriki kwenye nafasi za uongozi na kuchangia kuifikisha nchi katika dira ya maendeleo ya mwaka 2025 na kupunguza vitendo vya rushwa na ufisadi.
Mafunzo hayo yatakuwa endelevu kwa kundi hili ambapo itatolewa misukumo na hamasa namna ya wao kama nguzo pekee kuweza kujitokeza na kushiriki pamoja na kugombea nafasi mbalimbali kwenye chaguzi zijazo.
Post a Comment