Ads

Wanafunzi zaidi ya 100 Shule za Msingi kuchuana Mashindano ya Tahajia



Hussein Ndubikile
Mwamba wa habari
Wanafunzi kutoka Shule ya Zaidi 100 wa Mikoa ya Dar es Salaam, Lindi na kwa mara ya kwanza Visiwa vya Zanzibar watachuana katika Mashindano ya kutamka herufi za maneno ya Kiingereza (Tahajia) yanayotarajiwa kuhitimishwa Novemba 10 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Hayo yalibainishwa jana na Mkurugenzi wa Taasisi ya Coconut, Frank Mush ambapo alisema mashindano yamefunguliwa rasmi mwezi Agosti na kilele chake kitafikia Novemba mwaka huu huku akisisitiiza washindi kumi watakaopatikana wanatarajiwa kuwa mabalozi wa elimu ya usomaji wakitarajia pia kupata mialiko kuiwakilisha nchi kaitika ngazi za kimataifa.

" Shindano hili litashirikisha shule za Seriakli, binafsi na wadau wote wa elimu na umma kwa ujumla wake kwa mwaka huu yataanzia ngazi ya shule ambapo washindi 10 hupatikana kufuzu kimkoa," alisema Mushi.

Alibainisha kuwa kutokana nawingi wa shule , mkoa wa Dar es Salaam kupitia Manispaa za awali za kiutawala yaani Temeke, Ilala na Kinondoni zitafanya mashindano ya kimkoa hivyo kufanya mikoa 5 ukijumlisha Zanzibar na Lindi.

Mushi alisema washindi 20 kutoka kila mkoa watafuzu mashindano ya kitaifa ili kupata washindi 10 bora kutoka makundi mawili kulingana na ngazi za madarasa.

Alisisitiza kuwa mwaka huu Coconut Foundation imeungwa mkono na mdahamini Mkuu wa mwaka ambayo ni kampuni ya kuchapisha vitabu vya elimu ya ngazi zote ijulikanayo kama Oxford University Press Tanzania na kwamba Kituo cha Runinga cha ITV kitarusha mashindano hayo mubashara ili kuweza kumfikia kila mwananchi.

Alifafanua kuwa lengo la mashindano hayo ni kuifika mikoa yote huku akisisitiza kwa mwaka huu lugha ya Kiingereza itatumika peke yake.

Pia alisema usajili wa ushiriki utakoma  rasmi wiki ya pili ya mwezi Septemba hivyo taasisi inaendelea shule kujisajili kufanikisha shindano hilo.

Kwa upande wake, Meneja wa kampuni ya uchapishaji vitabu na kamusi nchini, Fatma Shangazi alisema wameamua kudhamini kutokana na umuhimu wake kwa watoto katika kuboresha uwezo wao wa kutamka na kusoma na kwamba zawadi za vikombe vitatolewa kwa washindi wa mwisho.

Naye Meneja Masoko wa Kituo cha ITV na Radio One, Ernest Dile alisema wataendelea kushirikiana na Coconut Foundation kufanikisha mashindano hayo huku akiziomba taasisi zingine kujitokeza kudhamini.

No comments