Ads

Manispaa Ya Kinondoni Yakabidhiwa Chuo Cha Ufundi.

 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Benjamin Sitta akielekezwa jambo


Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni leo imekabidhiwa rasmi Chuo Elimu  ya Ufundi Tegeta (TVTC)kilichopo madale jijini Dar es salaam na Shirika la Good Neighbours Tanzania na kuifanya halmashauri hiyo kuwa ya Kwanza nchini kumiliki chuo cha ufundi.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya Chuo hicho Mastahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Benjamin Sitta, amesema chuo hicho kitakuwa daraja muhimu katika kuendeleza sekta ya viwanda hapa nchini.

Amesema kuwa  kwa kutoa wataalama mbalimbali wa ufundi ambao wataifikisha Tanzania katika uchumi wa viwanda.

Mhe. Sitta amesema kuwa wanafunzi wote watakaohitimu katika chuo hicho wataunganishwa moja kwa moja na mikopo inayotolewa na halmashauri ya manispaa ya kinondoni.

"Tunautaratibu wa kutoa mikopo kwa vijana,wanawake na walemavu ili kuwawezesha kujiajiri sambamba na kuwatafutia eneo la kufanyia shughuli zao" amesema Mhe. Sitta.

Mkurugenzi wa shirika la GoodNeigbours Tanzania Bw Hunggoo Ann, amesema shirika hilo kupitia mradi wake wa elimu ya ufundi lilianzisha na kukiendesha chuo hicho miaka kumi iliyopita kwa madhumuni ya kusaidia upatikanaji wa elimu ya ufundi kwa jamii hasa vijana.

Amesema kuwa kwa sasa wameamua kukibidhi ili kuendeshwa rasmi na Serikali kupitia halmashauri ya manispaa Kinondoni.

Mkuu wa chuo hicho Bw Ignas Kisinde, ameiomba halmashauri hiyo  kukiendeleza vyema chuo hicho cha elimu ya ufundi huku akitaja upungufu wa walimu,majengo, vifaa vya kufundishia pamoja na kukosekana kwa gari la kusafirisha wanafunzi na watumishi.

Mpaka sasa wahitimu zaidi ya 747 wamehitimu masomo yao katika fani mbalimbali za ufundi na kufanikiwa kujiari na kuwajili.

No comments