Ads

Tuzo 32 za Tanzania Elimu Awards kushindaniwa Agosti 31 Dar es Salaam


Hussein Ndubikile
Mwamba wa habari
Jumla ya Washiriki 70 wakiwemo wanafunzi, walimu, shule, serikali, taasisi pamoja na wadau pamja na wadau wa elimu watachuana kuwania tuzo 32 za Tanzania Elimu Awards (TEA) zitakazotolewa na Kampuni ya Elimu Solutions Agosti 31 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Hayo yalibainishwa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa kamupi hiyo Neitahn Swed ambapo alisema wameamua kuanzisha tuzo hizo kwa mara ya kwanza kwa kutambua  na kutahamini mchango wa walimu na wanafunzi katika kujenga taifa bora wakati likielekea kwenye uchumi wa viwanda.

" Hafla ya kutoa tuzo hizi itafanyika tarehe 31 siku ya Jumamosi kuanzia saa 9 mchana mpaka saa 2 usiku  mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mheshimiwa Suleiman Jafo," alisema Swed.

Alibainisha kuwa TEA itatoa tuzo 32 kutoka kwenye vipengele 11 na kwamba vigezo vitakavyoangaliwa ni ufaulu wa mitihani ya kitaifa kuanzia ngazi ya elimu ya msingi hadi Kidato cha sita huku akisisitiza shindano hilo litakuwa endelevu.

Swed alisema washindi wa tuzo hizo watapatikana kutokana na takwimu zitakazopatikana kwa kushirikiana na wadau pamoja na Kamati waliyoichagua.

Alifafanua kuwa tuzo hizo zipo kwa ajili ya kuchangia utamaduni na kutunza na kutambua mchango wa wasomi, wabunifu na wadau kwenye sekta ya elimu hasa wakati nchi ikielekea uchumi wa kati kupitia uchumi wa viwanda.

Kwa upande wake, Mratibu wa TEA, Peter Mboye alivitaja vipengele vitakavyoshindaniwa vikiwemo vya wanafunzi bora wa kike na kiume ngazi ya msingi hadi kidato cha tano, wanafunzi bora kwa ujumla, walimu bora kwa msingi na sekondari, wanafunzi wenye mahitaji maalum, taasisi bora pamoja na wilaya zilizofanya vizuri katika ufaulu.

Naye Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni hiyo, Catherine Ndosi aliwashukuru wadau waliofanikisha tuzo hizo na kuziomba taasisi zingine kujitokeza kusapoti shindano hilo.

Mwakilishi kutoka Kampuni ya Asas, Abdul Ally alisema wameamua kudhamini tuzo kwa kuwa wanatambua umuhimu wa elimu na kwamba mwaka jana walitoa lita 300,000 kwa ajili ya kuboresha afya za wanafunzi wa Nyanda za Juu Kusini.

No comments