TCRA kampeni ya Mnada kwa Mnada Jijini Tanga katika utoaji wa Elimu ya Usajili wa laini kwa kutumia alama za vidole.
|
Wakazi
wa jijini Tanga na viunga vyake wamejitokeza kwa wingi katika
kampeni ya Mnada kwa Mnada ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA) ikishirikiana na Kampuni ya simu, Jeshi la Polisi Kitengo cha
Uhalifu Mitandaoni na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa
ajili ya utoaji wa huduma za usajili wa laini za simu kwa kutumia
vitambulisho vya kitaifa na kuhakikiwa na kampuni za simu kwa kuweka
alama za vidole kwa laini za simu.
Mkuu
wa Kanda ya Kaskazini wa TCRA Mhandisi Emelda Salum amesema ni fursa
kwa wananchi wa wa Tanga kupata huduma kutokana na kuwa na mnyororo
wadau wa mawasiliano.
Amesema Mnada kwa Mnada
utadumu kwa siku tatu katika Viwanja vya Tangamano jijini Tanga ambapo
itatoa fursa kwa wananchi wengi kufika kupata huduma za Mawasiliano na
usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.
Salum
kuwa kampeni ya Mnada kwa Mnada ni kwa ajili ya kutoa elimu ya
mawasiliano kwa kushirikiana na wadau katika kujibu changamoto
wanazokutanazo katika utumiaji wa mawasiliano nchini.
Salum
amesema kuwa wananchi wasio kuwa na Vitambulisho vya NIDA wahakikishe
wanapata katika usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole na
huduma nyinginezo za Mawasiliano hayo.
Amesema kuna
watu wengine wanatumia mawasiliano ya simu bila kujua ambapo Jeshi
Polisi lipo katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ili kuwaelewesha makosa ya
jinai ya matumizi ya simu.
Aidha amesema Kampeni
hiyo ni endelevu katika kuwafikia ikiwa kuhakikisha kila mwananchi
anajisajili laini yake kwa alama za vidole kwa kutumia kitambulisho cha
taifa cha NIDA.
Amesema kuwa TCRA iko kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi ili mtumie Mawasiliano kwa usalama kutokana na elimu tunayotoa.
Salum amesema kuwa wananchi wajitokeze katika kujisajili kwa alama za vidole kabla ya Desemba 31.
"TCRA
tumejidhatiti katika kuwafikia wananchi katika utoaji wa elimu za
utumiaji wa bidhaa za mawasiliano kwa kutatua changamoto katika huduma
hiyo"amesema Salum
Post a Comment