Meya Kumbilamoto awapa ofisi Wafanyabiashara mnada wa Pugu, aahidi kutatua kero zinazowakabili
Mwambawahabari
Wafanyabiasha ya mifugo katika mnada wa Pugu ,wameiomba Serikali kuboresha huduma za miundo mbinu ya mnadahuo ilikuondoa usumbufu wanaoupata katika kunyeshwa ,kushusha na kupandisha mifugo katika magari.
Wafanyabiashara hao wametoa ombi hilo mbele ya Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto alipofanya ziara ya kutembelea mnadahuo kusikiliza kero zao akiambatana na katibu wa CCM wilaya Ilala Idd Mkoa , ambapo ameahidi kuzitatua kero hizo huku akibaini udanganyifu katika baadhi ya vyanzo vya mapato.
"Mnazo changamoto za ofisi, nimewapa chumba hapa mtafanyiashughuli zenu humu ninyi ni Watu muhimu sana mnapatia mapato Manispaa, Nawaomba pia vijana mchangamkie fursa ya mikopo ya Halmashauri ili muweze kufanya biashara vizuri" alisema Kumbilamoto.
Akizungumza katika ziara hiyo kuhusu huduma hizo katibu wa CCM wilaya ya Ilala Idd Mkoa amesema kuwa, suala la miundombinu mbinu ya Mnadani hapo Lina muda mrefu yapata miaka 4,bivyo ameahidi kukifikisha kwa Katibu Mkuu wa CCM mkoa ili aweze kukifikisha Kuna Kong husika.
Kwaupande wake Meneja wa mnada huo Kerambo Samweli ,amesema wizara ya mifugo na uvuvi inazifahamu changamoto hizo na kusema kuwa zinafanyiwa kazi.
Nao baadhi ya wafanya biashara walipata fursa ya kuzungumza wamebainisha badhi ya changamoto zinazowakabili mnadani hapo, kuwa ni Pamoja na sehemu za kunywesha maji mifugo, Sehemu Kushusha na kupandisha mifugo kwa kuwa zilizopo hazimidhi mahitaji Kwani mifugo imekuwa ikivunjika.
Post a Comment