Ads

UVCCM WILAYA YA ILALA WATOA TAMKO KWA MABEBERU WA SIASA


NA HERI SHAABAN(PUGU)

UMOJA wa vijana wa UVCCM wilaya ya Ilala umeshauri uchaguzi wa Mkuu wa Rais na Wabunge unaotarajia kufanyika mwaka ,2020  Tume ya Uchaguzi ipitishe jina la Rais Magufuli  agombee peke yake mabeberu wa siasa hawana nafasi.

Mapendekezo hayo yalitolewa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wilaya ya Ilala Hamad Pazi wakati wa kongamano la Pugu ya Kijani Wilayani Ilala .

Pazi alisema  Mwenyekiti wa CCM Taifa katika utekelezaji wa Ilani ya chama UVCCM tunapendekeza katika uchaguzi huo lipitishwe jina moja la Rais Magufuli pekeyake anatosha kupeperusha bendera ya Chama mabeberu wa  wanaowania kiti hicho  hawana sifa.

"Nitazungumza na Wabunge wangu wa CCM waliopo wilayani Ilala  wapeleke sheria ya mpito Bungeni wakubali ili Tume ya Uchaguzi ipitishe jina moja la Magufuli  kwani aina haja kupitisha na wengine,"alisema  Pazi.

Pazi alisema Magufuli ni kiongozi mwenye chachu ya maendeleo katika uongozi wake amefanya mambo makubwa katika kuibadilisha nchi kuelekea Tanzania ya Viwanda.

"UVCCM wilaya ya Ilala tunamtambua Magufuli ndio Rais wa sasa mpaka 2025 watu wenye uchu wa madaraka  wakae chonjo waache juhudi za JPM ziendelee"alisema.

Aidha alisema mpaka sasa  mambo mengi makubwa yamefanyika Kupitia Serikali ya awamu ya tano wakati anaingia Madarakani  alisema serikalj yake itakuwa serikali yenye kuwajali watu wanyonge kuwakwamua watu wa hali yaChini.

Alisema katika juhudi za Magufuli ameanzisha mpango wa elimu bure  kuanzia Shule ya Msingi mpaka Chuo Kikuu.

Pia alisema hakuna Mtoto wa masikini  Nyumbani kwa kukosa ada  chini ya uongozi wake kwani elimu ni haki ya msingi ya kila mtoto wa Kitanzania sambamba na uboreshaji wa vituo vya afya ununuzi wa ndgege mpya na uboreshaji wa miundombinu ya barabara

Wakati huohuo katika mkutano kongamano hilo la Pugu ya Kijani imevuna vigogo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA  akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho Mtaa wa Kigogo Freshi Edwin Amatory  aliyeamia CCM

Aliwataka vijana wa kata hiyo kushirikiana na chama   pia wasiweke makundi yatakayowagawanya  badala yake wote wawe wamoja katika katika kuelekea chaguzi serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu
2020
Mwisho

No comments