Mbunge Bonah awataka Kisukuru kuchagua CCM
NA HERI SHAABAN(Kisukuru)
MBUNGE wa Segerea (CCM)Bonah Ladslaus amewataka wana CCM wa Kata ya Kisukuru kukichagua chama cha Mapinduzi CCM kwa ajili ya maendeleo.
Bonah alitoa ushauri huo Kata ya Kisukuru Wilayani Ilala leo ,wakati wa kikao chake na Viongozi wa CCM kuangalia uhai wa chama.
" Nawaomba wana CCM wenzangu chagueni CCM kwa ajili ya maendeleo kwani ccm ni chama kinacho tekeleza Ilani kwa wananchi "alisema Bonah.
Bonah aliwataka Wana CCM kukichagua chama hicho kwa ajili ya maendeleo katika chaguzi mbalimbali ikiwemo kushiriki chaguzi za Serikali za Mitaa Novemba mwaka huu na uchaguzi mkuu wa Rais 2020.
Aidha aliwataka wachague kiongozi bora kwa ajili ya kuleta maendeleo katika jimbo la Segerea na Wilaya ya Ilala kwa ujumla.
Aliwataka wananchi wake wa jimbo la segerea kuwa makini katika uchaguaji wa viongozi sio bora kiongozi wachague viongozi wenye chachu na maendeleo ya nchi yao.
Alitolea mfano kata za Kimanga na Kisukuru zimekosa maendeleo kwa viongozi wa kata hizo wameshindwa kusogeza huduma za jamii.
"Mmechagua viongozi lakini hawana msaada kwenu mfano kata ya Kisukuru aina soko wala Zahanati
Diwani wenu mliomchagua toka achaguliwe ajawai kufanya mkutano na wananchi wala kusoma mapato na matumizi alafu mnasema mna diwani kwa sasa Diwani wenu ni Ofisa Mtendaji ndio anashughulika na Wananchi" alisema
Aliwataka masuala ya Mikopo ya halmashauri waunde vikundi vyao Mtendaji atawasaidia na mama Maendeleo wa Kata wakikosa msaada wafike Ofisi ya Mkurugenzi Ilala ipo wazi watamuona Mama Maendeleo wa Wilaya kwani mikopo ni haki yao kila mtu akope na kupeleka marejesho ili wengine wakope.
Kwa upande wake Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kisukuru,Mohamed Bashiri alisema Kisukuru vikundi 55 vimeomba mkopo kati ya hivyo tisa vimeingiziwa fedha bado vikundi vingine vipo katika mchakato wa kupewa mikopo vikundi saba kutoka Mtaa wa Banebane.
Mwisho



Post a Comment