Ads

MHE. Mayeye : Wakinamama wajiandikishe daftari kupiga kura ili wagombee nafasi za uongozi.

Mbunge wa Viti Maalumu CUF-Kigoma Mhe. Kiza Mayeye akizungumza na waandishi wa habari.
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Wakinamama wametakiwa kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa Serikali za mtaa kwa kujiandikisha katika daftari la kupiga kura pamoja na kugombea nafasi za uongozi katika chaguzi mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Makamo Mwenyekiti wa  JUKE Mhe. Kiza Mayeye, amesema kuwa ni vizuri wakinamama wakajiandikisha katika daftari la kupiga kura kwa sababu ni haki yao ya kikatiba.

Amesema kuwa kujiandika katika daftari  la kupiga kura watapata fursa ya kuchagua viongozi watakaosimamia maslai ya kinamama katika kuondokana na umaskini katika jamii.

"Tunataka wakinamama tukachague viongozi watakaotusaidia kuondokana na umasikini, utegemezi pamoja na kuhakikisha tunapiga hatua katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo" amesema Mhe. Mayeye.

Mhe. Mayeye ni Mbunge wa Viti Maalumu CUF-Kigoma, ameeleza kuwa wamekuwa wakifanya jitiada za kuwajengea uwezo wakinamama kitu ambacho kimewasaidia kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali.

Amesema kuwa wakinamama hawapaswi kukata tamaa katika kutafuta maendeleo katika jamii, huku akisisitiza kuwa katika uchaguzi wajitokeze Kuna kupiga kula.

Katika hatua nyengine amebainisha
kumemakuwa changamoto ya kutokuwa nafasi ya kufanya mikutano ya hadhara kwa ajili ya kutoa elimu kwa wakinamama.

"Kukosekana kwa mikutano ya hadhara ni changamoto kwetu kutokana ninakosa nafasi ya kufikisha ujumbe" amesema Mhe. Mayeye.

No comments