Ads

CCM YASHINDA NAFASI YA MEYA ILALA

Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akipiga kula katika baraza la madiwani la halmashauri ya Ilala Julai 31/2019 (Picha na Heri Shaaban)

NA HERI SHAABAN,DAR ES SALAAM.
MADIWANI wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala leo wamemchagua Omary Kumbilamoto kuwa Meya wa Manispaa ya Ilala kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM)

Kabla kushika nafasi hiyo  Omary Kumbilamoto alikuwa Naibu Meya wa Halmashauri ya Ilala.

Awali Halmashauri hiyo ilikuwa ikiongozwa na Meya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Charles Kuyeko ambaye alijiuzuru nafasi hiyo .

Baraza hilo la kikao uchaguzi lilifunguliwa na  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ilala Jumanne Shauri kwa kusoma ajenda za kikao kisha Baraza likafunguliwa na Msimamizi wa uchaguzi Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Sheila Edward .

Akifungua baraza hilo  Sheila Edward alisema jumla ya Madiwani wote waliofika idadi yao wapiga kura 55 uchaguzi ulianza Omary Kumbilamoto alijiuzuru Nafasi ya Naibu Meya akagombea Umeya Wajumbe wakamtea   Mbunge Abdalah Burembo kuwa Mwenyekiti wa muda .

Wabunge wote wa CCM walishiriki uchaguzi huo akiwemo Mbunge wa Ukonga Mwita Waitara  CCM,Mbunge wa Ilala Mussa Zungu , Mbunge wa Segerea Bonah Ladslaus, Stella Ikupa,Janeth Masaburi.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Sheila Edward alisema  uchaguzi ulikuwa mzuri jumla ya wapiga 55 kura , wagombea CCM walimsimamisha Omary Kumbilamoto  Diwani wa Vingunguti,CHADEMA walimsimamisha Diwani wa Kinyerezi Greyson Selestin .

Sheila alisema katika uchaguzi huo amna kula iliyoaribika  Omary Kumbilamoto ameibuka mshindi  amepata kula 41 CCM na Greyson Selestine amepata kula 14 CHADEMA .

Akizungumza mara baada kuibuka kwa ushindi mnono Omary Kumbilamoto alimpongeza Mwenyekiti wa CCM Taifa John Magufuli kwa kumpa ridhaa kugombea nafasi hiyo na sasa amekuwa Meya wa Ilala.

Kumbilamoto alisema awali alikuwa Naibu Meya wa Ilala katika wadhifa wake mpya atajenga mahusiano mazuri na Viongozi wa Ofisi ya Mkuu  wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema pamoja na Ofisi ya Mkuu wa mkoa Paul Makonda.

"Mmenipa ridhaa kwa kunichagua dhamira yangu nitawatumikia katika kusimamia Serikali ya Wilaya ya Ilala pamoja na kusimamia miradi ya maendeleo yote ya Serikali"alisema Kumbilamoto

Naye Mbunge wa Ukonga CCM Mwita Waitara alipongeza uongozi wa CCM kuchagua Meya wa Chama cha Mapinduzi wa Ilala wote sasa CCM ,amewataka sasa wafanye kazi  Ilala ife safi zaidi.

No comments