Ads

MANISPAA YA ILALA YADHIMISHA WIKI YA UNYONYESHAJI DUNIANI


NA HERI SHAABAN, DAR ES SALAAM.
MANISPAA ya Ilala imezindua wiki ya unyonyeshaji maziwa ya Mama kwa Mtoto.

Madhimisho hayo yanafanyika kila mwaka mwezi Agosti Tanzania huungana na nchi nyingine Duniani kuadhimisha wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Ofisa Lishe wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Frola Mgimba, alisema malengo ya wiki ya unyonyeshaji Duniani mwaka 2019 kuinua uelewa wa jamii kuhusiana na jamii kuhusu jinsi ya usawa wa kijinsia sheria na kanuni,zinazowezesha kulinda ,kuendeleza na kusaidia unyonyeshaji maziwa ya mama na hivyo kuberesha usawa wa kijinsia katika ngazi zote ili kusaidia kulinda na kuendeleza na kusaidia unyonyeshaji.

Aidha Frola alisema malengo mengine ya siku hii kuimiza uimalishaji wa usawa wa kijinsia ,usimamizi na utekelezaji wa sheria na kanuni zinazosaidia kulinda  ,kuendeleza na kusaidia unyonyeshaji wa maziwa ya mama na hivyo kuboresha lishe ya jamii.

Alisema wiki hii ya unyonyeshaji inaanza Agosti mosi hadi Agosti 7 kila mwaka na mwaka huu kauli mbiu ya maadhimisho hayo "Waweshe Wazazi kufanikisha Unyonyeshaji ".

Akielezea baadhi ya faida ya unyonyeshaji wa Maziwa ya Mama kwa Watoto ni unyonyeshaji wa maziwa ya mama huchangia kwa kiasi kikubwa katika kuboresha afya ,kulinda uhai wa maisha ya mtoto ,kunyonyesha maziwa pekee katika miezi sita ya mwanzo ya maisha ya mtoto ndio njia bora na salama ya kumpatia mtoto virutubisho vyote muhimu kwa ukuaji na maendeleo yake.

Alitaja faida zingine maziwa ya mama yana  sifa ya kipekee ya kuwa na kinga mwili ambazo umkinga mtoto dhidi ya magonjwa mbalimbali hivyo kuchangia katika kupunguza vifo vya watoto wachanga na walio katika umri wa miaka mitano.

Frola alisema kunyonyesha pia kuna faida kubwa kwa mtoto kunajenga mahusiano katika ya mama na mtoto hivyo kumjenga mtoto kijamii zaidi.

Aliwataka wazazi mara baada ya kujifungua Mama na mtoto anashauriwa wagusane ngozi kwa ngozi ,wanyonyeshe mtoto ndani ya saa moja baada ya kujifungua .

Pia Mama anashauriwa ndani ya miezi sita usimpe maji au vyakula vingine badala yake mtoto mama unashauriwa kumpa maziwa pekee kwa miezi sita.

No comments