SERIKALI KUBORESHA COCO BEACH.
Mwambawahabari
Na Grace Semfuko-MAELEZO
Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango
imetoa jumla ya shilingi Bilioni 28 kwa Wilaya ya Kinondoni, Jijini
Dar Es Salaam kwa ajili ya kuendeleza miradi miwili ikiwepo ujenzi wa
soko la Tandale na uboreshaji kwa kuendeleza ufuukwe wa Osterbay, maarufu
Coco Beach, lengo likiwa ni kulipa thamani eneo hilo na kuongeza watalii
wa ndani nan je.
Utiaji saini kwa ajili ya mkataba wa ujenzi huo ulifanywa
February 4 mwaka huu, kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dotto
James na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Aron Kagulumjuli, ambapo
kati ya fedha hizo shilingi Bilioni 14 zitaendeleza Ufukwe wa Osterbay,
eneo la Coco Beach na zingine Bilioni 14 zitajenga Soko la Tandale.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo aliyasema
hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya mazingira ya “Mchanga Pekee”
iliyo na lengo la kubadilisha mazingira ya fukwe za bahari ya Hindi,
jijini Dar Es salaam, iliyofanyika leo asubuhi kwenye ufukwe wa Coco,
zoezi lililoambatana na usafi wa mazingira kwenye eneo hilo.
“Wilaya yangu ya Kinondoni tumekuja na mpango maalum
wa kuimarisha mazingira ya Bahari, tunazo Bilioni 28 kwa ajili ya miradi
miwili ya kuimarisha mazingira; zikiwemo fukwe za Osterbay zinazojumuisha
eneo hili la Coco pamoja na kuimarisha mazingira ya soko la Tandale”
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Chogolo Wanavikoba wa Buguruni na taasisi
mbalimbali zilizofika kushiriki.
Akisikilizwa na karibu mamia ya watu, wengi wao wakiwa
akina mama wa vikoba, Bw. Chongolo alisema zoezi lililopo sasa ni hatua
ya kutangaza mzabuni kwa ajili ya ujenzi huo ambapo katika kipindi cha
miaka miwili ijayo shughuli hiyo itaanza.
Mbali na fedha hizo za miradi miwili, Serikali mwaka
jana ilitoa zaidi ya shilingi Bilioni 9 kwa ajili ya ukarabati wa soko
la Magomeni, Jijini Dar Es Salaam zoezi ambalo linaendeleo mpaka sasa,
aidha Chongolo alitoa wito kwa jamii kuhusu kuendeleza na kuzitunza
fukwe za bahari ili kutengeneza mazingira mazuri ya wananchi kupumzika
pia kubarizi
Naye Afisa Uhusiano Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania
– TTB, Geofrey Tengeneza alisema fukwe za Bahari ni maeneo muhimu
kwani watalii wengi wa ndani na nje ya nchi hutembelea maeneo hayo na
hivyo yanahitaji kutunzwa katika hali ya usafi.
“Fukwe hizi ni muhimu sana kwa utalii katika nchi
yetu, hivyo tunahitaji kuzitunza na tusichafue mazingira ya fukwe zetu”
alisema Tengeneza na kusisitiza kuwa ufukwe wa Coco ni maarufu kwa watu
wote na serikali inatambua hilo na kwamba utaendelea kutumiwa na watu
wote kwa ajili ya kupumzika na burudani.
Kampeni ya “Mchanga pekee” imeanzishwa na Kampuni
ya Cocacola kwanza na inalenga kuboresha mazingira ya fukwe za Bahari
na kuwa safi na Cocacola inashirikisha Bodi ya Utalii Tanzania pamoja
na mashirika na taasisi mbalimbali nchini.
Kampeni hiyo imekuja kufuatia ripoti ya Shirika la
“International Council of Beverages Associations (ICBA)” iliyotolewa
mwishoni mwa mwaka 2018 ikionesha uchafuzi mkubwa wa fukwe za bahari
duniani kufikia wastani wa vipande vya plastiki kilomita elfu 13 na
kubainika kuwepo kwa tani milioni 150 za plastiki kwenye fukwe hizo
mpaka leo.
Mkurugenzi Mkuu wa Cocacola, Bazil Gadzios leo alisisitiza
kuwa kampeni hiyo inalenga kufanya usafi kwenye fukwe
wa Coco Beach, kukusanya chupa za plasitiki elfu kumi kila mwezi, kutoa
elimu kwa jamii kuhusu kuhifadhi mazingira ya fukwe za bahari, kupunguza
chupa hizo pamoja na kuhifadhi ekolojia ya viumbe vya Baharini na nchi
kavu.
Post a Comment