REPSSI YAENDELEA NA KAMPENI KUTOKOMEZA MIMBA NA NDOA ZA UTOTONI
Mkurugenzi Mkazi wa Repssi Tanzania, Edwick Mapalala akiongea na vijana kijiweni kuhusu athali za mimba
.................................................................
Shirika
linalojihusisha na masuala ya kijamii na kisaikolojia kwa watoto
(REPPSI) limeendelea kufanya kampeni ya kutokomeza tatizo la ndoa na
mimba za utotoni mkoani Pwani.
Kampeni
hiyo inafanyika ili kuhakikisha watoto wa kike wanatimiza ndoto zao za
kielimu ili kushiriki katika mkakati wa Serikali wa Tanzania ya viwanda.
Akizungumza
na wakazi wa Kibiti Mkoani Pwani, Mkurugenzi Mkazi wa REPSI Tanzania,
Edwick Mapalala alisema tatizo la mimba na ndoa za utotoni bado kubwa na
kwamba linahitaji jitihada za pamoja kupambana nalo.
“Mfano
ni hizi kampeni za kutoa elimu na kuihamasisha jamii kumthamini mtoto
wa kike zinasaidia kwa hiyo kama tutaendelea nazo jamii itaelewa, watoto
watatimiza ndoto zao,” alisema.
Mapalala
alisema katika kampeni hizo wanazoshirikiana na Shirika la Pasada
linalojihusisha na masuala ya Ukimwi chini ya Kanisa Katoliki Jimbo Kuu
la Dar es Salaam na Pwani, vijana hasa madereva bodaboda wamefikishiwa
elimu kuhusu thamani ya mtoto wa kike.
Baadhi ya viongozi wa vijiji na kata walikiri kuwa ndoa za utotoni ni changamoto kubwa lakini wanaendelea kupambana nayo.
Mratibu
wa Elimu Kata ya Salala, Wilayani Kibiti Erasmus Assenga alisema kwa
mwaka huu tu wanafunzi wawili wa Sekondari katika kata hiyo wameacha
masomo kwa mimba.
“Kwa
hiyo kampeni hii ni muhimu kwa sababu watoto wa kike wenyewe
wanafikishiwa elimu, jamii hasa wanaume wanaelezwa na wanajua umuhimu wa
kuwathamini,” alisisitiza.
Kwa
upande wake Afisa Ustawi wa Jamii wa Pasada Ester Mbwana alisema
anaamini kuwa baada ya kampeni hizo kutakuwa na mafanikio makubwa kwa
sababu, jamii inaelewa na imekubali kusaidia katika ulinzi wa mtoto.
Post a Comment